Makardinali 133 wapiga kura wamewasili Roma na mada nyingi zinajadiliwa
Vatican News
Jumatatu tarehe 5 Mei 2025, Makardinali wameendelea na mkutano wa kumi katika kujiandaa kwa ajili ya Mkutano Mkuu ujao wa uchaguzi wa Papa mpya na kuendeleza mijadala yao kuhusu hali ya Kanisa na matumaini yao ya siku zijazo. Msemaji mkuu wa Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican, Dk. Matteo Bruni, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatatu kwamba Makardinali 179, wakiwemo makardinali 132 wapiga kura, walishiriki katika Mkutano Mkuu wa kumi. Katika taarifa yake alibainisha kwamba Makardinali wote wapiga kura 133 wapo mjini Roma, kabla ya mkutano utakaoanza Jumatano tarehe 7 Mei 2025.
Kwa upande wa Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Baraza la Makardinali, aliliambia Baraza la Makardinali kwamba, Kardinali Camerlengo, Kevin Farrell, walipiga kura Jumamosi mchana kwa ajili ya shughuli za vyumba vya Makardinali. Wote watakuwa katika Nyumba ya Mtakatifu Marta na ile ya zamani ya Mtakatifu Marta mjini Vatican.
Kwa mujibu wa Dk Bruni, alieleza pia kuwa Makardinali wapiga kura wataweza kusafiri kutoka Nyumba ya Mtakatifu Marta kwenda kwenye kikanisa cha Sistine kama wanavyotaka, hata kwa miguu, lakini kwa njia inayolindwa. Katika mkutano kulikuwa na maingiliano 26 ya mijadala Jumatatu asubuhi hii ambayo iligusia mada zifuatazo: “Sheria ya Kanoni na jukumu la Mji wa Vatican; - Hali ya kimisionari ya Kanisa; Nafasi ya Caritas katika kutetea maskini; Uwepo wa waandishi wa habari wengi ulisisitizwa, ulionekana kama ishara kwamba Injili ina maana katika ulimwengu wa leo - kama wito wa kuwajibika; Maombi wakati wa janga la UVIKO ilikumbukwa, kama mlango wazi wa tumaini wakati wa hofu.”
Na kuhusu Papa mpya ilijadiliwa: “wingi wa wanatumaini kuwa na mchungaji wa karibu na watu, lango la Umoja; wa kukusanya kila mtu katika damu ya Kristo, katika ulimwengu ambapo utaratibu wa kimataifa huko katika mgogoro; Changamoto za kusambaza imani, kutunza kazi ya uumbaji, vita, na ulimwengu uliogawanyika vipande vipande.” Kadhalika kama hiyo haitoshi, mjadala wa “wasiwasi ulioeshwa juu ya migawanyiko ndani ya Kanisa; Wajibu wa wanawake katika Kanisa, katika muktadha wa sinodi; Miito, familia, na elimu ya watoto ilishughulikiwa; Kurejea kwenye hati za Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatikan, hasa Dei Verbum, yaani uliojikita na Neno la Mungu kwa jinsi Neno la Mungu lilivyo lishe kwa watu wa Mungu.”
Dk. Bruni alisema juhudi zote zinafanywa katika Mikutano Mikuu ili kuhakikisha Makardinali wote wanaotaka kuzungumza wanapata fursa ya kufanya hivyo. Kazi imekamilika zaidi kwenye kikanisa cha Sistine na vile vile katika malazi kwenye Nyumba mbili za Mtakatifu Marta na Makardinali wanaweza kuingia kuanzia Jumanne asubuhi. Waandishi wa habari, alisema Bw. Bruni, hawataweza kutembelea kikanisa cha Sistine, kwa kuwa Maaskari wa Vatican tayari wanakililinda. Hata hivyo, alibainisha, picha zitatolewa zinazoonesha mambo ya ndani yaliyoandaliwa.
Maoni