Mkutano wa Makardinali wa 11 ulifanyika na kiapo kwa wasaidizi wa mkutano mkuu
![]() |
walitoa kiapo cha usiri kabisa. (ANSA)Conclave: maofisa na wahusika wengine walitoa kiapo cha usiri kabisa. (ANSA) |
Vatican News
Mkutano wa 11 wa makardinali ulifanyika saa kumi na moja jioni kwa kufunguliwa na sala ya pamoja. Walikuwapo makardinali 170, miongini mwake makardinali 132 wa kupiga kura. Mijadala kama 20 hivi ilijihusiana na mada kubwa ya umuhimu wa kichungaji na kikanisa. Muda ulitolewa kwa suala la ukabila ndani ya Kanisa na katika jamii. Uhamiaji ulijadiliwa, kwa kutambua wahamiaji kama zawadi kwa Kanisa, lakini pia kusisitiza uharaka wa kusindikizana nao na kuunga mkono imani yao katika miktadha ya uhamaji na mabadiliko. Mara kadhaa, vita vinavyoendelea vilitajwa, mara nyingi vikiwa na sauti zilizooneshwa na ushuhuda wa moja kwa moja wa makardinali kutoka kanda zilizoathiriwa na migogoro.
Safari ya Sinodi juu ya kisinodi ilijadiliwa tena, ikionekana kama kielelezo halisi cha kikanisa cha ushirika, ambapo kila mtu ameitwa kushiriki, kusikiliza na kung’amua kwa pamoja. Dhamira na wajibu wa Makardinali wa kumuunga mkono Papa mpya ulithibitishwa tena, na kuitwa kuwa mchungaji wa kweli, kiongozi anayejua kuvuka mipaka pekee ya Kanisa Katoliki pekee, kukuza mazungumzo na kujenga uhusiano na ulimwengu wa kidini na kiutamaduni. Changamoto iliyowakilishwa ya kuenea kwa madhehebu mengi katika sehemu mbalimbali za dunia ilikumbukwa pia. Vile vile kulikuwa na kula kiapo cha viongozi wakuu na wafanyakazi wa Mkutano huo Mkuu wa uchaguzi(Conclave),makuhani na walei, katika Kikanisa cha Pauline, katika Loggia ya Kwanza ya Jumba la Kitume. Kikao kiliisha saa 1:00 jioni masaa ya Ulaya. Mkutano Mkuu wa kumi na mbili wa Makardinali ulipangwa kufanyika tarehe 6 Mei 2025 asubuhi.
Kutamka kiapo cha usiri kamili
"Ninaahidi na kuapa kuweka usiri kamili na mtu yeyote ambaye si sehemu ya Baraza la Makardinali Wapiga kura, na hii daima, isipokuwa nipate kitivo maalum kilichotolewa na Papa mpya aliyechaguliwa au warithi wake, kuhusu kila kitu kinachohusiana moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na kupiga kura na uchunguzi kwa ajili ya uchaguzi wa Papa Mkuu." Hiyo ndiyo kanuni, iliyotamkwa ya usiri kamili pia katika siku zijazo kuhusu kile kinachotokea katika Jiji la Vatican, wakati wa Mkutano Mkuu, na hasa kuhusu kile "kinachohusiana na shughuli za uchaguzi wa Papa mpya; kuheshima marufuku kwa vifaa vya kurekodia sauti na video, chini ya adhabu ya kutengwa na latae sententiae ikiwa na maana ya sheria ya Kanoni ya kutengwa… iliyohifadhiwa kwa Kiti cha Kitume. Haya ndiyo maudhui ya kiapo kilichotolewa tarehe 5 Mei 2025, katika Kikanisa cha Pauline, kama ilivyoelekezwa na Universi Dominici Gregis, yaani Katiba ya Kitume iliyotangazwa na Papa Yohane Paulo II kunano tarehe 22 Februari 1996. Kitachukuliwa na "wale wote watakaohusika katika Mkutano mkuu ujao, wote kikanisa na na walei waliokubaliwa na Camerlengo Kardinai na wasaidiz wake watatu.
Mbali na Katibu wa Baraza la Makardinali na Msheherejaji wa Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa, Askofu Mkuu Diego Ravelli, wafuatao walikuwepo: Wasimamizi 7 wa sherehe za Kipapa; Padre aliyechaguliwa na Kardinali anayesimamia Mkutano Mkuu ili, kumsaidia katika kazi yake; watawa wawili wa Mtakatifu Augustino waliokabidhiwa Sakrestia ya Kipapa; watawa wa lugha mbalimbali kwa ajili ya maungamo; madaktari na wauguzi; waendeshaji lifti za Jumba la Kitume; wafanyakazi waliopewa huduma ya chakula na huduma za kusafisha; wafanyakazi wa kupamba maua na Huduma za Kiufundi; waliopewa kazi ya kuwasafirisha wapiga kura kutoka nyumba ya Mtakatifu Marta hadi kwenye Jumba la Kitume; Kanali na Mkuu wa Kikosi cha Uswisi cha Ulinzi wa Kipapa aliyepewa kazi ya uangalizi karibu na Kanisa la Sistine; mkurugenzi wa Huduma za Usalama na Ulinzi wa Raia wa Mji wa Vatican akiwa na baadhi ya washirika wake. Baada ya kuelekezwa juu ya maana ya kiapo hicho, wote walitamka na kusaini kibinafsi kanuni iliyotakiwa, mbele ya Kardinali Kevin Joseph Farrell, Camerlengo wa Kanisa Takatifu la Roma, na Wawakilishi wawili wa Kitume kama idadi ya Mashahidi Washiriki.
Maoni