MTEULE THE BEST Kwako Mheshimiwa Rais, Kwanza kabisa nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuongoza taifa hili la Tanzania na pia pole kwa majukumu uliyonayo,kuna mengi mazuri unayafanya huenda sisi watanzania wa kawaida hatuyaelewi na kuona unakosea ila naamini mwisho wa siku tutaelewa. Lengo la ujumbe huu kwako ni kuhusiana na kilio tulichonacho sisi vijana ambao kwa muda sasa tunasubiri ajira. Ni muda wa miezi 9 umepita tangu uliposema mbele ya vyombo vya habari kuwa zoezi la uhakiki litadumu mwezi mmoja na nusu haitozidi miwili utakuwa umetoa ajira ambapo wengi tukawa tuna matumaini kuwa zitatoka ajira zile 71,000 lakini mpaka leo kwa taarifa mzitoazo ni kuwa mmetoa ajira 5000 kuachia mbali za wakurugenzi na wenyeviti wa taasisi mbalimbali. Si kweli kwamba vijana wote ni wavivu na tumeshindwa kujiongeza la hasha kinachopelekea tuonekane wazembe, hatuwezi kujiongeza,mizigo kwa wazazi,hatutaki kujiajiri sababu kubwa ni hizo ahadi zenu mnazotupa za miezi miwili miwili...