Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KAMPUNI

Mabadiliko ndani ya Simba SC Tanzania ni muamko mpya?

Mmiliki mwenza wa Simba SC Mohammed Dewji anijtahidi kuona klabu hiyo inakuwa ndani na nje ya uwanja (Picha kwa hisani ya Mahmoud Bin Zubeiry) Siku ya Jumanne mashabiki wa mojawapo wa timu kongwe Tanzania watakusanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kusherehekea "Simba Day". Ni katika kuidhinisha wiki ya Simba au kwa umaarufu "Simba Week" na inahusisha mechi ya kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya Zambia pamoja na mechi za timu za wanawake walio chini ya miaka 20. Shughuli zilizopangwa kwa siku saba zimenuiwa kuongeza ukaribu na ushirikiano baina ya wachezaji na mashabiki wa timu hiyo pamoja na Simba kuisaidia jamii kupitia miradi tofuati. Ni sehemu ya azimio la Bilionea Mohammed Dewji, mmiliki mwenza wa klabu hiyo anayeitaka klabu hiyo ikuwe ndani na nje ya uwanja ili kuhakikisha ufanisi zaidi. "Niliwahi kukutana na mojawapo ya viongozi wa Zamalek (mnamo 2003) na niligundua wakati huo kuwa bajeti ya Zamalek ni mara 50 zaidi ya baj...