Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 29, 2020

SIMIYU YAJIPANGA KUPAMBANA NA COVID-19

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema  mkoa umetenga shule za Sekondari za Bweni za Serikali kuwa maeneo ambayo yatatumika kuwahifadhi washukiwa wa Virusi vya Corona  endapo watapatikana mkoani hapa;  baada ya serikali  kufunga shule na vyuo nchini kwa siku 30 lengo likiwa kukabiliana na ugonjwa huo. Mhe. Mtaka ameyasema hayo wakati akipokea mchango kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya  shule ya sekondari Anthony Mtaka uliotolewa na umoja wa madhehebu ya kikirsto Lamadi na kuongeza kuwa mbali na maeneo ya shule Mkoa pia umetenga maeneo ya hoteli ambayo yatatumika endapo washukiwa/watu wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huo ambao hawatahitaji kukaa kwenye maeneo ya shule. "mkoa hautatumia hoteli kwa ajili ya kuhifadhi mtu yeyote atakayeshukiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona badala yake tutatumia shule za zetu za sekondari za bweni lakini ikitokea mtu anahitaji kukaa hotelini tayari tumeandaa hoteli za kutosha"alisema Mtaka. " ...