BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) mkoa wa Mwanza limerejesha umiliki wa kiwanja namba 111 kitalu T kilichopo Kenyatta Road jijini hapa kwenye eneo maarufu la 'Muslim' (ilipo stendi ya Igombe) kilichokuwa kimechukuliwa na halmashauri ya Jiji la Mwanza. Bakwata imerejesha umiliki huo baada ya kushinda kesi kufuatia halmashauri ya Jiji la Mwanza kushindwa kutimiza masharti iliyopewa na mahakama. Shauri hilo namba 150 ya mwaka 2020 lililotokana na kesi namba 58 ya mwaka 2017 liliamuliwa Juni 3, 2022 ambapo Mahakama ilithibitisha kwamba kiwanja hicho ni mali halali ya Bakwata. Akitoa taarifa kwa umma wa kiislam leo Juni 5, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bakwata jijini Mwanza, Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Hasani Kabeke amesema katika uamuzi wake mahakama ilitoa masharti mawili kwa halmashauri ya Jiji ikitakiwa kulipa fidia ili kukitwaa kiwanja hicho ama irudishe kiwanja hicho kama fidia itashindwa kufikiwa ndani ya miezi mitatu, ambapo...