Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya WIZI

Korea Kaskazini 'yaiba mabilioni kutengeza makombora'

Korea Kaskazini inasema jaribio la hivi karibuni la makombora yake ni onyo kwa Marekani na Korea Kusini Korea Kaskazini imeiba dola bilioni mbili (£1.6bn) kufadhili mpango wake wa silaha kupitia uvamizi wa kimtando, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyovuja. Ripoti hiyo ya kisiri inasema Pyongyang inalenga mabenki na na ubadilishanaji wa sarafu ya crypto-currency kukusanya pesa. Vyanzo vya habari vimethibitishia BBC kwamba UN ilikuwa ikichunguza mashambulio 35 ya kimtandoa. Korea Kaskazini ilifyetua makombora mawili siku ya Jumanne ikiwa ni mara ya nne imechukua hatua hiyo katika kipindi cha chini ya wiki mbili Katika taarifa, Rais wa nchi hiyo Kim Jong-un amesema hatua hiyo ni onyo dhidi ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini. Pyongyang imeelezea kuwa mazoezi hayo yanakiuka mkataba wa amani. How could war with North Korea unfold? Ripoti t iliyovuja na ambayo ilitumwa kwa kamati ya vikwazo vya Korea Kaskazini katika Baraza Kuu...

Msanii wa The Mafik akamatwa kwa wizi

Msanii wa kundi la The Mafik anayejulikana kwa jina la Mbalamwezi, amekamatwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni kwa tuhuma za wizi. Wasanii wanaounda kundi la The Mafik, Hamadai (kushoto) Mbalamwezi (kati kati) na Rhino (kulia) Tukio hilo limetokea hapo jana baada ya msanii huyo kumuibia dereva wa gari ya moja ya kampuni zinazotoa huduma za usafiri binafsi jijini Dar es salaam (Taxify), aliyejulikana kwa jina la Calvin. Akisimulia tukio hilo Calvin amesema Mbalamwezi aliitisha usafiri akitumia simu ya mwenzake, lakini alipokuwa njiani alionekana kuwapigia simu watu kuomba hela kwani hakuwa na pesa ya kumlipa dereva, na ndipo alipochukua uamuzi wa kumuibia dereva baada ya kumfanya apoteze fahamu. Meneja wa kundi la The Mafik aliyejitambulisha kwa jina la Kapasta amesema ni kweli kuna hilo tukio, lakini ndio yuko njiani akielekea kituo cha Polisi Oysterbay ambako msanii huyo amewekwa rumande ili ajue kinachoendelea. East Africa Television ilifanya jitihada za kumtafuta Kama...