Jumapili hii imekuwa ya kihistoria kwa wanawake wa Saudi Arabia Wanawake nchni Saudi Arabia rasmi sasa wameruhusiwa kukaa kwenye usukani, baa ya miongo kadhaa kutopata ruhusa hiyo Mabadiliko haya yalitangazwa mwezi Septemba mwaka jana na Saudi Arabia ikatoa leseni za kwanza kwa wanawake mwanzoni mwa mwezi huu. Ilikuwa nchi pekee iliyobaki duniani ambapo wanawake walikuwa hawaendeshi magari na familia zao zilikuwa zinakodisha dereva kwa ajili ya wanawake. Hata hivyo, hatua hii imefikiwa wakati kukiwa na Kampeni ya kuwakamata wanaharakati ambao wamekuwa wakipaza sauti wapatiwe haki ya kuendesha magari. Takriban wanaharakati wa haki za wanawake wanane wanashikiliwa na huenda wakafikishwa mahakamani na kupatiwa kifungo kwa uanaharakati wao, Shirika la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International limeeleza. Miongoni mwa wanaoshikiliwa ni pamoja na Loujain al-Hathloul, mwanaharakati kinara katika kampeni hiyo. Amnesty pia imetaka kufanyiwa mabadiliko makubwa ...