Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 14, 2019

IRAN YALIPIZA KISASI YAKAMATA MELI YA UINGEREZA

Iran yakamata meli ya Uingereza eneo la Ghuba Kutakuwa na 'madhara makubwa''ikiwa Iran haitaachia meli ya mafuta ya uingereza wanayoishikilia, Waziri wa mambo ya kigeni Jeremy Aunt ameeleza. wamilili, Stena Impero kuwa wameshindwa kufanya mawasiliano na meli hiyo. Kamati ya dharura ya serikali hiyo, cobra, anakutana kwa ajili ya kuzungumzia jambo hilo. Bwana Hunt amesema kitendo hicho ''hakikubaliwi kabisa. ''Tunajua wazi kuwa hali hii haitakuwa rahisi kuitatua, kutakuwa na madhara makubwa,'' alisema. ''hatuangalii suluhu ya kijeshi.Tunatafuta suluhu ya kidiplomasia kutatua hali hii, lakini tunajua tunapaswa kushughulikia.'' Amesema wafanyakazi ndani ya meli walikuwa wa mataifa tofauti tofauti lakini hakuna raia wa Uingereza aliykuwa akifahamika kuwa ndani ya chombo hicho. Chombo cha kampuni ya Stena Impero ilikuwa ikisafiri majini ikiwa na bendera ya Uingereza na kusajiliwa London. ''Balozi wetu mjini Tehran anf...

TANZANIA YAIKOSOA BENKI YA DUNIA

Ni kwanini Tanzania imekosoa makadirio ya benki ya dunia ya ukuaji wa uchumi wake Albina Chuwa, mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) Taasisi ya takwimu nchini Tanzania imesema kuwa inaweza kutathmini takwimu za ukuaji wa uchumi wake wa mwaka 2018 baada ya Benki ya dunia kutoa takwimu zilizoonyesha kiwango cha chini cha ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo. Waziri wa fedha wa Tanzania aliliambia bunge mwezi uliopita kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kilikuwa ni 7% mwaka jana. Benki ya dunia ambayo ilitoa hesabu zake kwa misingi ya data za taifa , matarajio ya mwaka 2019 ya ukuaji wa kiwango cha 5.4% - pia ilitoa kiwango cha chini cha ukuaji chini ya kile kilichokuwa kimekadiriwa na na serikali cha 7.1%. Albina Chuwa, mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ametetea njia zake na namna alivyofikia kiwango hicho, Reuters linaripoti. "Tumekwenda kote nchini kukusanya data halisi , sio sawa na mtu ambaye anakaa Washington na kutengeneza sampuli za pato la ndani ...

MAREKANI YALIPIZA KISASI KWA IRAN

Raisi wa Marekani Donald Trump amesema jeshi la maji la Marekani limetungua ndege isiyo na rubani ya Iran katika eneo la mpaka kati ya ghuba ya uajemi na ghuba ya Oman. Amesema meli ya jeshi lake ''ilichukua hatua'' siku ya Alhamisi baada ya ndege hiyo kusogea kwa takriban mita 914 karibu na chombo hicho. Iran haijasema chochote kuhusu hilo. Mwezi Juni, Iran iliangusha ndege ya kijeshi isiyo na rubani ya Marekani, na kusababisha hofu ya kutokea mzozo wa kijeshi. Awali Tehran ilisema imekamata ''meli ya kigeni'' na wafanyakazi wake 12 siku ya Jumapili kwa kusafirisha mafuta kinyume cha sheria. Iran imekuwa ikishutumiwa na Marekani kwa kushambulia meli zake tangu mwezi Mei.Tehran ilikana shutuma hizo. Raisi Donald  Trump  amesemaje ? Akizungumza Ikulu, Trump amesema ''Ninataka kuwajulisha kuhusu tukio lililotokea kwenye eneo la mpaka wa Hormuz leo lililohusisha meli yetu ya kijeshi. Chombo hicho kilichukua hatua ya kujilinda dhidi ya nde...

Magazeti ya leo Ijumaa Julai 19 2019

 MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 19 2019  

S-400 Yaleta gumzo NATO kuwa makombora hatari zaidi dunia

Nato yaitaka Urusi kuheshimu mkataba wa silaha Marekani ilikasirishwa na hatua ya Urusi kuipatia Uturuki mfumo wa makombora ya masafa marefu Muda unakwisha wa kuunusuru mkataba muhimu wa Urusi, katibu Mkuu wa wa muungano wa Nato Jens Stoltenberg amiambia BBC. Bwana Stoltenberg ameahidi kuwa zitachukuliwa hatua "zilizopangwa na za kujilinda " kama Urusi haitarejea katika utekelezaji wa mkataba ifikapo tarehe 2 Agosti ambao ni muda wa mwisho uliowekwa. "lazima tujiandae kwa ajili ya dunia... Kutokana na makombora zaidi ya Warusi ," amesema Kiongozi wa Muungano wa kujihami la nchi za magharibi-NATO makubaliano ya 1987 yaliyosainiwa baoina ya Marekani na Muungano wa Usoviet USSR yalipiga marufuku makombora ya masafa mafupi na marefu. Rais Trump alitangaza kuwa Marekani itaacha utekelezaji wa majukumu yake chini ya mkataba juu ya vikosi vya masafa vya nuklia mwezi Februari, ikiishutumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo. Urusi inakana madai hayo, lakini ilisitish...

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 16.07.2019

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 16.07.2019:Maguire, Neymar, Bruce, Fernandes, Alderweireld, Coutinho Leicester imemwambia mlinzi wake wa kati Harry Maguire, 26, kuwa anaweza kuondoka (Telegraph) Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27, amerejelea kauli yake uhusu nia yake ya kuondoka kwenye klabu hiyo kwenye mkutano wake na mkurugenzi wa ufundi Leonardo . (ESPN) Newcastle watalipa pauni milioni 4 kama fidia kwa timu ya Sheffield Wednesday kwa ajili ya kocha wao wa zamani Steve Bruce.(Sun) Wasaidizi wa Bruce Steve Agnew na Stephen Clemence pia wameondoka Sheffield Wednesday na watajiunga naye St James'Park .(Newcastle Chronicle) Manchester United watapeleka rasmi ofa ya kumnasa kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 24, katika kipindi cha majuma matatu yajayo. Mkurugenzi wa Roma Gianluca Petrachi amethibitisha kuwa klabu yake ina mpango wa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Tottenham Toby Alderweireld, 30. (Football Italia) Alderweireld na mchezaji ...

Mambo yako vipi kwa Air Tanzania hii leo?

Air Tanzania: Faida ikoje baada ya kufufuliwa shirika la ndege Tanzania? Ndege ya Dreamliner ilipowasili Tanzania Julai 2018 Wiki hii shirika la ndege nchini- Air Tanzania linaidhinisha njia mpya ya usafiri - jambo linalotazamwa kuwa fursa ya ukuwaji linapokuja sula la usafiri wa abiria. Rais John Pombe Magufuli aliahidi kwamba shirika hilo litaimarishwa na ndege mpya kununuliwa mara baada ya kuingia madarakani. Tanzania, kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Zambia, Zimbabwe, Nigeria na Uganda, imelifufua shirika lake la ndege, ama kama lijulikanavyo, Air Tanzania. Uwekezaji mkubwa umefanywa mpaka sasa katika kulifanikisha hilo. "Shirika letu la ndege lilikuwa na hali mbaya sana, lilikuwa na ndege moja tu tena ilikuwa inafanyiwa matengenezo mara kwa mara, soko la ATCL lilishuka sana hadi kufikia asilimia 2.5. Lakini sasa tumenunua ndege 7, na nyingine kubwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner itakuja mwaka 2020", alisema Rais Magufuli mwaka jana 2018 katika  hafla ya ...