Iran yakamata meli ya Uingereza eneo la Ghuba
Kutakuwa na 'madhara makubwa''ikiwa Iran haitaachia meli ya mafuta ya uingereza wanayoishikilia, Waziri wa mambo ya kigeni Jeremy Aunt ameeleza.
wamilili, Stena Impero kuwa wameshindwa kufanya mawasiliano na meli hiyo.
Kamati ya dharura ya serikali hiyo, cobra, anakutana kwa ajili ya kuzungumzia jambo hilo.
Bwana Hunt amesema kitendo hicho ''hakikubaliwi kabisa.
''Tunajua wazi kuwa hali hii haitakuwa rahisi kuitatua, kutakuwa na madhara makubwa,'' alisema.
''hatuangalii suluhu ya kijeshi.Tunatafuta suluhu ya kidiplomasia kutatua hali hii, lakini tunajua tunapaswa kushughulikia.''
Amesema wafanyakazi ndani ya meli walikuwa wa mataifa tofauti tofauti lakini hakuna raia wa Uingereza aliykuwa akifahamika kuwa ndani ya chombo hicho.
Chombo cha kampuni ya Stena Impero ilikuwa ikisafiri majini ikiwa na bendera ya Uingereza na kusajiliwa London.
''Balozi wetu mjini Tehran anfanya mawasiliano na wizara ya mambo ya kigeni wa Iran kutatua hali hii na tunafanya kazi kwa karibu na washirika wetu wa kimataifa,'' alisema.
Tukio hili limefanyika wakati kukiwa na mvutano kati ya Uingereza, Marekani na Iran.
Jeshi limesema meli hiyo imekamatwa kwa kuvunjwa kwa sheria tatu: kuzima GPS; kuingia kwenye mpaka kupitia njia ya kutokea badala ya kuingilia; na kupuuzia maonyo.
Taarifa zinasema hakuna taarifa zozote kuhusu majeruhi na usalama wa wafanyakazi ni jambo la kwanza kwa wamiliki na mameneja.
Tarehe 9 mwezi Julai, Uingereza ilieleza tishio la usalama katika maji ya Iran kwenye Ghuba ni ''kubwa''.
Wakati huohuo, Marekani imedai kuwa imedungua ndege isiyo na rubani kwenye Ghuba, baada ya Iran kushambulia ndege isiyo na rubani katika eneo hilo mwezi Juni.
Raisi wa Marekani Donald Trump amesema atazungumza na Uingereza kufuatia madai kuwa Iran imeikamata meli iliyosajiliwa nchini Uingereza.
Iran imekuwa ikishutumiwa na Marekani kufanya mashambulizi dhidi ya meli katika maeneo muhimu ya usafirishaji tangu mwezi Mei. Tehran imekana shutuma zote.
Mzozo kati ya Marekani na Iran umeshika kasi tangu Marekani ilipoongeza vikwazo dhidi ya Iran baada ya kuamua kujitoa kwenye mkataba wa nyukilia wa Iran wa mwaka 2015
Maoni