Ruka hadi kwenye maudhui makuu

S-400 Yaleta gumzo NATO kuwa makombora hatari zaidi dunia






Nato yaitaka Urusi kuheshimu mkataba wa silaha



Marekani ilikasirishwa na hatua ya Urusi kuipatia Uturuki mfumo wa makombora ya masafa marefu

Muda unakwisha wa kuunusuru mkataba muhimu wa Urusi, katibu Mkuu wa wa muungano wa Nato Jens Stoltenberg amiambia BBC.

Bwana Stoltenberg ameahidi kuwa zitachukuliwa hatua "zilizopangwa na za kujilinda " kama Urusi haitarejea katika utekelezaji wa mkataba ifikapo tarehe 2 Agosti ambao ni muda wa mwisho uliowekwa.

"lazima tujiandae kwa ajili ya dunia... Kutokana na makombora zaidi ya Warusi ," amesema Kiongozi wa Muungano wa kujihami la nchi za magharibi-NATO

makubaliano ya 1987 yaliyosainiwa baoina ya Marekani na Muungano wa Usoviet USSR yalipiga marufuku makombora ya masafa mafupi na marefu.


Rais Trump alitangaza kuwa Marekani itaacha utekelezaji wa majukumu yake chini ya mkataba juu ya vikosi vya masafa vya nuklia mwezi Februari, ikiishutumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo.

Urusi inakana madai hayo, lakini ilisitisha kwa muda utekelezaji wa majukumu yake ya mkataba huo muda mfupi na baadae kutangaza mipango ya kutengeneza mfumo wa silaha za nuklia.


Kiongozi wa Muungano wa Usovieti Mikhail Gorbachev na rais wa Marekani Ronald Reagan walisaini mkataba wa udhibiti wa makombora ya kijeshi mwaka 1987

Katika mahojiano mahojiano ya kina na BBC, Bwana Stoltenberg anasema Makombora ya Urusi - ambayo anasema ni "ukiukaji wa wazi wa mkataba" - yanauwezo wa kinuklia, kutumika popote, ni magumu kuyatambua, na yana uwezo wa kuifikia miji ya Uolaya katika kipindi cha dakika chache.

"Hili ni tatizo kubwa. Mkataba wa udhibiti wa matumizi ya nuklia umekuwa muhimu katika udhibiti wa silaha kwa karne kadhaa na sasa tunashuhudia kukiukwa kwa mkataba," alisema.

Huku kipaumbele kilikuwa nu kuirejesha Urusi kuheshimu kanuni za mkataba , Bwana Stoltenberg amesema ''hakuna ishara zozote " kuwa nchi hiyo itafanya hivyo. "kwa hiyo tunapaswa kujiandaa kwa ajili ya dunia bila makataba wa udhibiti wa silaha na kwa jaili ya makombora zaidi ya Urusi ."

NATO; hatutaki mzozo na Urusi



Huku NATO ikiwa haina mpango wa kupeleka makombora yake nuklia ya ardhini yaliyoko Ulaya, Bwana Stoltenberg amesema kuwa Muungano huo utajibu kwa kiwango " kilichopimwa, kwa njia ya kujilinda" ikiwa Urusi itakataa kurejea katika utekelezwa wa mkataba ifikapo tarehe 2 Agosti.

Makombora ya ulinzi , mafunzo mapya na utayari wa wanajeshi , na udhibiti wa silaha mpya , kwa pamoja vinaweza kuwa ni sehemu ya namna NATO itakavyoingilia kati, alisema. Uamuzi wowote wa mwisho utachukuliwa baada ya muda wa mwisho uliowekwa kwa Urusi kurejea kwenye mkataba.


Katibu Mkuu wa wa muungano wa Nato Jens Stoltenberg amiambia BBC kuwa unakwisha wa kuunusuru mkataba muhimu wa na urusi

Bwana Stoltenberg pia amezungumzia juu ya suala la Urusi kuwasilisha mfumo wa makombora ya masafa wa kiwango cha juu wa ulinzi S-400 kwa mjumbe wa Nato, Uturuki wiki hii.

Marekani inasema kuwa itaiondoa Uturuki kwenye mpango wake wa uingiliaji kati wa ndege za mapigano za -F-35 fighter jet, kujibu hilo. Serikali ya Ankara hivi karibuni imekuwa karibu sana na utawala wa Moscow nchini Urusi , suala linaloibua hali ya wasi wasi kati ya Uturuki na marekani.

NATO yamuonya Trump kuhusu uamuzi dhidi yake



" Ni tatizo kubwa kwasababu ni makubaliano ya maana ambayo yanahusisha washirika muhimu wawili ," amesema Bwana Stoltenberg. Nato inaunga mkono juhudi za kumaliza mzozo juu ya mkataba , aliongeza, huku akisifu mchango wa Uturuki katika muungano wa Nato.


Mara kwa mara rais Donald Trump amekuwa akiwatolea wito wanachama wa Nato kuchangia fedha zaidi katika muungan

Katibu mkuu wa Nato pia alisifu juhudi miongoni mwa wajumbe za kuongeza malengo ya bajeti zao kwa kiwango cha 2%. Rais wa Marekani Donald Trump ametoa wito wa mara kwa mara wa kuwataka wajumbe kutoa mchango zaoidi kwa muungano wa Nato katika miaka ya hivi karibuni.

"Tumekata kona -hali ni bora zaidi kuliko ilivyokuw amiaka michache tu iliyopita, na nina matumaini makubwa kwamba washirika wa muungano wataendelea kuwekeza zaidi ," amesema. Nchi nane wanachama wa muungano huo wanatarajiwa kufikia malengo yao ya mchango mwaka 2019.




Hivi karibuni zaidi, Bwana Trump alizitolea wito washirika wa Nato kuepuka kutumia teknolojia iliyotolewa na kampuni ya teknolojia ya Uchina Huawei, akisema kampuni hiyo ni hatari kwa usalama- jambo ambalo Uchina inalikanusha.

Bwana Stoltenberg amesema kuwa muungano wa Nato unandaa miongozo mipya kukabiliana na suala hilo, ili wajumbe waweze kuwa na "viwango vilivyokubaliwa au miongozo ya namna ya kukabiliana na changamoto hizi ". Amesisitiza Stoltenberg


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...