CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeziandikia barua Marekani na Ujerumani kuzitaka kuziangalia tuhuma zilizoelekezwa dhidi yao za kukihusisha na chama hicho katika kile kinachodaiwa kuwa ni mipango ya kuhatarisha usalama wa Tanzania. Barua mbili za Chadema ambazo zimeandikwa Machi mosi mwaka huu na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari cha chama hicho, Tumaini Makene, zimetaka balozi za nchi hizo nchini kujibu tuhuma hizo ambazo zilielekezwa na Cyprian Musiba aliyejitambulisha kama Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI. Gazeti hili ambalo limefanikiwa kuona barua hizo jana, Chadema kimesema kimeona umuhimu wa kuchukua hatua hiyo ili kupata mwitikio wa nchi hizo juu ya tuhuma hizo nzito ambazo zinatakiwa kuangaliwa zaidi. Katika barua yenye kumbukumbu No. C/HQ/ADM/KS/24/02 ambayo imeelekezwa kwa John Espinos ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Uchumi, Ubalozi wa Marekani, Chadema imeeleza kwamba Februari 25, mwaka huu mtu aliyejulikana kwa jina la Cyprian Musib...