Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Diamond

Diamond Platnumz na ATCL: Mwanamuziki azozana na Air Tanzania kuhusu kuachwa na ndege uwanjani Mwanza

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Diamond Platnumz ametofautiana na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuhusu kilichotokea hadi akaachwa na ndege uwanjani mwanza. Mwanamuziki huyo anasema tamko lililotolewa na shirika hilo kwamba alichelewa kufika uwanjani si za kweli. ATCL kupitia taarifa wamesema Diamond , ambaye wamemrejelea kama Isaack Nasibu, alikuwa miongoni mwa abiria waliopaswa kusafiri na ndege ya shirika hilo Jumapili 16 Desemba, 2018 hakuachwa kama inavyodaiwa bali alichelewa kufika uwanjani kwa muda unaotakikana. Anadaiwa kufika dirishani robo saa baada ya dirisha kufungwa. Jina rasmi la mwanamuziki huyo ni Nasibu Abdul Juma Issaack. "Kampuni inapenda kutoa ufafanuzi kuwa abiria huyo alifika uwanjani kwa kuchelewa na hivyo kuzuiliwa na mamlaka zinazosimamia uwanja kwa mujibu na taratibu," ATCL wamesema. Aidha, shirika hilo la serikali limepuuzilia mbali madai ya msanii huyo kwamba tiketi yake iliuzwa kwa abiria wengine. "Kampuni inapenda kutoa ufaf...

Diamond hatimaye hapata mpenzi mpya

Tanasha Donna Oketch: Mkenya huyu 'anayependwa' na mwanamuziki Diamond Platnumz ni nani hasa? Mwanamuziki nyota wa Tanzania Diamond Platnumz ametangaza kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kwamba yuko katika uhusiano wa kimapenzi na Mkenya, au si uhusiano? Platnumz amepakia video kuashiria kwamba yuko kwenye mahaba na dada kwa jina Tanasha Donna Oketch. Bi Oketch, ni mtangazaji katika kituo cha redio cha NRG nchini Kenya. NRG ni miongoni mwa vituo vipya vya redio nchini Kenya ambavyo vimekuwa vikilenga kuwavutia zaidi vijana. Diamond, ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul Juma, kwenye video ya Insta Stories Jumanne aliandika kuwa: "Maskini simba yuko kwenye mapenzi…Mmwamini, yupo kwenye mapenzi." Mwanamuziki huyo kwa utani hujiita Simba au Chibu Dangote. Video inayoonyesha vivuli vya wanaoaminika kuwa yeye na Tanasha wakitembea ufukweni inaonesha ujumbe wa "I love you Tanasha" (Nakupenda Tanasha) ambayo yameandikwa mchangani. Diamond, ambay...

Naibu Waziri wa madini ataka taarifa za utafiti wa madini zitolewe kwa Wananchi

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida kuhakikisha unatoa taarifa za tafiti zake zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ili wachimbaji wadogo waweze kuzitumia katika kubaini madini yaliyopo na kuanza kuchimba kwa kufuata sheria na kanuni za madini.  Naibu Waziri Biteko alitoa agizo hilo jana tarehe 19 Novemba 2018 kwenye mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi wilayani Ikungi mkoani Singida kama sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wachimbaji wa madini  Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mazingira bora ya uchimbaji  wa madini kwa wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa mbalimbali za utafiti zilizofanywa na Wakala wa Utafiti na Jiolojia Tanzania (GST) na kampuni za utafiti wa madini lengo  likiwa ni kuhakikisha kuwa uchimbaji wao unakuwa...

Mwaka mchungu na mtamu kwa Diamond

Toka mwaka 2009 hadi sasa Diamond Platnumz amekuwa akifanya vizuri kimuziki na kipindi chote hicho ameweza kushinda tuzo za ndani na za kimataifa pia. Kabati lake lina tuzo kubwa zaidi ya 10 kama Channel O Music Video Awards, HiPipo Music Awards, MTV Europe Music Awards/WORLDWIDE ACT AFRICA/INDIA, MTV Africa Music Awards, African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) na nyinginezo.  Kwa mwaka huu amefanya mengi makubwa na mazuri ingawa amekuwa na changamoto kubwa kwake.Chini nimeweka yale aliyofanikiwa na yale yalimpatia changamoto kwa huu.  1. Muziki Wake   Ni mwaka ambao Diamond Platnumz amejikuta nyimbo zake tatu zikifungiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Diamond hakuwa msanii wa kufungiwa lakini mwaka huu upepo huo umempuliza vilivyo.  February 28, 2018 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Nyimbo hizo ni zile ambazo hazikupaswa kuchezwa kwenye vyombo vya habari....

Makala: Achana na Wasafi Festival; Diamond, Alikiba hadi Studio

Huwenda nyakati zikawalazimu Diamond Platnumz na Alikiba kuwa kitu kimoja kwenye muziki kwa sasa. Ni kipindi kirefu wameripotiwa kutoelewa ingawa hakuna taarifa za uhakika kuhusu hilo.  Kwa sasa Diamond yupo katika pilika pilika za kuhakikisha tamasha lake la Wasafi Festival linafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Wakati akieleza kuhusu ujio wa Wasafi Festival alieleza kuwa angetamani na Alikiba angekuwepo kitu ambacho kiliibua mjadala mpana zaidi.  Alikiba tayari amekubaliwa kuwa sehemu ya udhamini wa Wasafi Festival kupitia kinywaji chake cha Mo Faya. Wengi wamesema huu ni mwanzo nzuri kwa wasanii hawa kurudisha ushirikiano wao na kufanya vitu vikubwa zaidi.  Kwanini Studio    Hapo jana Diamond Platnumz akiwahojiwa na kipindi cha Mambo Mseto cha Citizen Radio nchini Kenya alisema si Alikiba kushiriki Wasafi Festival tu bali hata kufanya wimbo pamoja yupo tayari.  "sio tu Alikiba mtu yeyote ambaye anahisi kuna sehemu nikimuweka Diamond itanisaidia katika k...

Diamond Platinumz: Daylan ni mwanangu halisi 'msiniletee

Msanii wa Tanzania Diamond Platnumz amewapuuzilia mbali wanaodhania kwamba yeye sio baba wa kweli wa mtoto wake wa kiume wa mwanamitindo Hamisa Mobetto. Diamond alichapisha ujumbe mkali katika mtandao wake wa Instagram akithibitisha kuwa Daylan ni mwanawe anayempenda sana. Hatua hiyo inajiri baada mwanamuzilki huyo kuchapisha kanda fupi ya video akivumisha ziara yake ya Marekani. Kanda hiyo fupi ya video inamuonyesha Diamond akizungumza kuhusu kazi yake na familia. Anazungumzia vile atakavyokuwa mbali na familia yake kwa takriban mwezi mmoja suala litakalomfanya kutowaona dada zake, mamake na watoto wake. Kanda hiyo ya video hatahivyo iliwaonyesha wanawe wawili aliyozaa na mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan. Video hiyo haikumuonyesha mwana wa Hamissa Mobetto, hatua iliowakera mashabiki wake waliotoa hisia tofauti kabla ya Diamond kuchapisha ujumbe huu. ''Huyu ni mwanangu... na ataendelea kuwa mwanangu maisha yangu yote, tena kipenzi changu... .Hakuweza kuwepo kweny...

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni

Diamond Platnumz Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video iliyosambaa kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa kitandani akicheza na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto pia na mwanamke mwingine ambaye hajajulikana,picha zinazoelezwa kuwa hazina maadili. Waziri wa habari,sanaa na michezo Dokta Harrison Mwakyembe amewaambia wabunge ni matokeo ya sheria mpya za mitandao zilizopitishwa mapema mwezi uliopita. Awali serikali ilitaja changamoto kubwa inayolikabili taifa ni athari ya utamaduni wa nje katika maadili, mila na desturi za Mtanzania kutokana na kuwepo na muingiliano mkubwa wa watu duniani. Ruka ujumbe wa Instagram wa angelasamwel Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa angelasamwel ''Kuna baadhi ya wasanii wetu ambao wamekuwa wakifanya uhuni uhuni ndani ya mitandao jana tumeweza kumkamata mwanamuziki nyota Diamond tumemfikisha polisi na anahojiwa kutokana na picha al...