Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Diamond hatimaye hapata mpenzi mpya

Tanasha Donna Oketch: Mkenya huyu 'anayependwa' na mwanamuziki Diamond Platnumz ni nani hasa?


Mwanamuziki nyota wa Tanzania Diamond Platnumz ametangaza kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kwamba yuko katika uhusiano wa kimapenzi na Mkenya, au si uhusiano?


Platnumz amepakia video kuashiria kwamba yuko kwenye mahaba na dada kwa jina Tanasha Donna Oketch.

Bi Oketch, ni mtangazaji katika kituo cha redio cha NRG nchini Kenya.

NRG ni miongoni mwa vituo vipya vya redio nchini Kenya ambavyo vimekuwa vikilenga kuwavutia zaidi vijana.


Diamond, ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul Juma, kwenye video ya Insta Stories Jumanne aliandika kuwa: "Maskini simba yuko kwenye mapenziā€¦Mmwamini, yupo kwenye mapenzi."

Mwanamuziki huyo kwa utani hujiita Simba au Chibu Dangote.

Video inayoonyesha vivuli vya wanaoaminika kuwa yeye na Tanasha wakitembea ufukweni inaonesha ujumbe wa "I love you Tanasha" (Nakupenda Tanasha) ambayo yameandikwa mchangani.

Diamond, ambaye amevuma kwa nyimbo kama vile Number One, Sikomi, Mawazo, Kamwambie, Nana, Mdogo Mdogo, na Ntampata Wapi, anasikika akisema: "Anapendeza hata kivulini." Mwanamuziki huyo amekuwa na tamasha kubwa la muziki la Wasafi Festival eneo la Mtwara, mji wa pwani ulio kusini mashariki mwa Tanzania.

Mwanamuziki huyo pia amewashirikisha wanamuziki wengine katika nyimbo maarufu kama vile Kwangwaru, Zilipendwa, African Beauty, Make Me Sing na wa karibuni zaidi Mwanza akiwa na Rayvanny ambao umefungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).

Ruka ujumbe wa Instagram wa tanashadonna

Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa tanashadonna


Mwanamuziki huyo kwenye video yake ya Instagram ameonekana kuwakosoa wapenzi wake wa awali akisema: "Hawakunichukilia kwa uzito. Nilipowahitaji, walinipuuza. Eti mimi ni mtu wa kuwachezaā€¦lakini yeye ameniamini...!"

Bi Oketch mwenyewe bado hajazungumzia taarifa hizi za uhusiano baina ya wawili hao hadharani, jambo linaloibua maswali kuhusu iwapo kweli ni mapenzi, au 'kutafuta'.

Kwenye Instagram, picha zake za karibuni zaidi zimeonekana kupigia debe NRGTAKEOVER, inayoonekana kuwa kipindi cha redio ambapo wasikilizaji watakuwa wakizawadiwa.


Katika ujumbe mmoja, ameandika: "Chilling here waiting on that #NRGTAKEOVER like.." (Nimetulia hapa nikisubiri #NRGTAKEOVER hiviā€¦"

Je, kuna uwezekano kwamba video za Diamond ni za kuvumisha kipindi hicho au labda kitu kingine wanachofanya kwa ushirikiano?

Hilo litabainika kadiri siku zinavyosonga! Mapenzi wenyewe walisema hayafichiki.

Tanasha Donna Oketch ni nani?

Jina lake kamili ni Tanasha Donna Barbieri Oketch lakini pia wakati mwingine mitandao ya kijamii hujiita Zahara Zaire.

Amezaliwa na wazazi wa asili mbili, Mkenya na Mwitaliano na amekuwa mwanamitindo kwa kipindi kirefu.


TANASHA DONNA

Alikulia Kenya hadi alipokuwa na miaka 11 alipohamia Ulaya nakupata fursa ya kushiriki katika shughuli za mitindo ya mavazi na maonesho mbalimbali.

Ameshiriki katika mashindan mbalimbali yakiwemo Miss Africa Belgium lakini aliambia chombo kimoja cha habari kwamba alitaka kurejea "nyumbani" na kushiriki shindano la Miss World Kenya, ndipo awakilishe taifa lake la kuzaliwa.

Akiwa Ubelgiji, alisomea somo la utalii.

Anaweza kuzungumza lugha tano ambazo ni Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kiholanzi na Kihispania.


Ingawa jamaa zake wengine wanaishi Kenya, mamake alisalia Ubelgiji, na kwa mujibu wa mtandao wa Tapmagonline, kwa sasa ana umri wa miaka 22 hivi.

Tanasha pia ni mwigizaji na mwanamuziki na ana kampuni yake ya nywele kwa jina 'For Her Luxury Hair' ambayo ndiye mwanzilishi wake na afisa mkuu mtendaji. Ni kampuni huuza nywele za binadamu.

Bi Oketch alikuwa na uhusiano na mwigizaji Mkenya, Nick Mutuma, ambaye jina lake kamili ni Nicholas Munene Mutuma.

Uhusiano wao ulifikia tamati mwanzoni mwa mwaka 2017, ambapo Bi Oketch alisema kwamba walikuwa watu "wasiopatana na wasiochukuana" na ndio maana wakaachana.

Ruka ujumbe 2 wa Instagram wa tanashadonna

Mwisho wa ujumbe 2 wa Instagram wa tanashadonna


Bi Oketch, alishirikishwa kama video vixen kwenye video ya wimbo wa Ali Kiba na Christian Bella kwa jina "Nagharamia".

Mapema mwaka huu, alipuuzilia mbali tetesi kwamba alikuwa na uhusiano na mwanamuziki huyo.

"Kiba na mimi wakati mmoja tulifanyia kazi video ya muziki, lakini hatujawahi kuwa na uhusiano," alisema kwenye Instagram.

Kiba aadaye alifunga ndoa na Mkenya Amina Khaleef.


Baada ya video za Diamond kupakiwa Instagram, wafuasi wake wamekuwa wakimfuata kwa wingi Bi Oketch na kumuandikia ujumbe mbalimbali katika ukurasa wake ambapo kufikia sasa ana wafuasi zaidi ya 107,000.

Alitangaza kwamba atakuwa na kipindi cha redio katika kituo cha NRG akiwa pamoja na DJ Kace Aprili mwaka huu.

Diamond Platnumz na Kim Nana, Zari na wengine

Diamond kwa muda alikuwa na uhusiano na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto.

Zari aeleza sababu za kumtupa Diamond

Hii ni baada ya uhusiano wake wa awali na raia wa Uganda Zari Hassan, ambaye ni mama wa watoto wake wawili kufikia kikomo Siku ya Wapendanao Februari mwaka huu.

Baada ya kuhusishwa kwa muda na Hamisa, Diamond alijitokeza na kusema kwamba hakuwa na uhusiano na mwanamke yeyote.

Kuna utata kwa sasa ikizingatiwa kwmaba mapema mwezi huu mamake Diamond, Sanura Kassim, alikuwa amethibitisha kwamba mwanawe alikuwa na uhusiano na mwanamke kwa jina Kim Nana, ambaye jina lake halisi ni Lilian Kessy.


Kim Nana ni video vixen pia, na mamake Diamond aliashiria kwamba mwanawe huyo amemshawishi mwanamke huyo kubadili hata dini yake kutoka Ukristo hadi Uislamu, wakijiandaa kufunga ndoa.

Diamond aliwahi pia kuwa na uhusiano na Miss Tanzania wa mwaka 2006 wema Sepetu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...