Aliyekuwa Rais wa 41 wa Marekani George H.W. Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94 huko mjini Houston, msemaji wake Jim McGrath amethibitisha kifo chake.
George H.W. Bush
Rais huyo wa zamani wa Marekani aliongoza kwa awamu moja tu akiingia madarakani mwaka 1989 na kuondoka 1993 hivyo kubaki kama Rais pekee aliyeiongoza Marekani kwa awamu moja.
Chanzo cha kifo cha George Bush hakijawekwa wazi rasmi, lakini Rais huyo mstaafu wa Marekani, kwa muda mrefu alikuwa akipambana na ugonjwa wa 'Vascular Parkinsonism', na kifo chake kimetokea ikiwa imepita miezi michache tangu mke wake Barbara Bush afariki dunia mnamo April 17, 2018 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa zaidi zinasema kwamba George Bush alikumbwa na ugonjwa huo tangu miaka ya 90, na mwenyewe aliwahi kuulezea kuwa ni ugonjwa mzuri kuupata kwani haumuumizi, isipokuwa tu anashindwa ku-'move' pale anapotaka hata kunyanyua mguu.
"Unaathiri miguu, hauumii, unaiambia miguu yako ijongee na haijongei, ni ajabu, lakini iwapo una ugonjwa mbaya, huu ni mzuri kuwa nao", alinukuliwa George Bush akizungumza alipokuwa akihojiwa na jarida la Parade mwaka 2012.
Kwenye maisha yake George Bush ameweka historia ya kuwa waziri Mkuu wa kwanza ambaye alikuwa madarakani kuchaguliwa kuwa Rais, na mtu wa pili kwenye utawala wa Marekani kushuhudia mtoto wake akichukua wadhifa huo, baada ya mtoto wake George Walker Bush kuwa Rais wa 43 wa Marekani.
George Bush alizaliwa huko Massachusetts Juni 12, 1924, akiwa mtoto wa tajiri na mfanyakazi wa Benki ya Wall Street na Senetor wa jimbo la Connecticut, Prescott Bush na mke wake Dorothy Bush.
George Bush ameacha watoto watano wakiwemo aliyekuwa Rais wa 43 wa Marekani, George Walker Bush, Jeb Bush, Dorothy Bush Koch ambaye ndiye mtoto wake wa kike pekee aliyebaki, baada ya mdogo wake Pauline Robinson Bush kufariki dunia akiwa na miaka minne, Neil Bush na Marvin Bush.
Maoni