Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 8, 2018

Luis Enrique kocha mpya wa Uhispania

Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ameteliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uhispania Kocha  wa  zamani  wa  klabu  ya  Barcelona  Luis Enrique ametia saini mkataba  wa  miaka  miwili  kuchukua  hatamu za kuifunza  timu ya  taifa  ya  Uhispania. Anachukua  nafasi  ya  Julen lopetegui, ambaye  alifutwa  kazi katika  mkesha  wa  kuanza  kwa  fainali  za kombe  la  dunia  baada  ya  kukubali kazi katika  timu  ya  Real Madrid. Fernando Hierro alichukua  udhibiti wa  timu  hiyo  kwa  muda  kwa ajili  ya  fainali  hizo, ambapo  mabingwa  hao  wa  mwaka  2010 wa kombe  la  dunia  waliondolewa  katika  awamu  ya  mtoano na wenyeji Urusi

Maoni: Malumbano ya Brexit yazidi London

Kama Uingereza itashindwa kufafanua kuhusu ni nani anayeongoza utaratibu na kutoa maamuzi muhimu kuhusu Brexit, Umoja wa Ulaya utalazimika kuendelea kusubiri tu. Kwanza, Waziri anayehusika na masuala ya Brexit David Davis alijiuzulu, kisha Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni na aliyeongoza kampeni za kuitaka Uingereza kujiondoa Ulaya Boris Johnson akafuata. Wanalivuruga jaribio la Waziri Mkuu Theresa May la kuishawishi serikali yake kukubali Uingereza kuendeleza mahusiano ya karibu na Umoja wa Ulaya baada ya Brexit. Kujiuzulu huko kulikoratibiwa kwa mawaziri hao wenye misimamo mikali kuhusu Brexit kunaitumbukiza serikali ya May katika mgogoro na kuvuruga matumaini ya Umoja wa Ulaya ya kuweza hatimaye kuanza, katika wiki chache zijazo, mazungumzo muhimu kuhusu makubaliano ya kutengana na mahusiano ya usoni kati ya Uingereza na umoja huo. Ni Ijumaa iliyopita tu ambapo May alijaribu, kulazimisha kuliunganisha baraza lake la mawaziri linalozozana. Lakini kama mambo yanavyokwend...

Wilshere ajiunga na West Ham, Torreira na Guendouzi 'waelekea' Arsenal

Mchezaji wa zamani wa Arsenal Jack Wilshere amejiunga na klabu ya West Ham kwa mkataba wa miaka mitatu na kusema kuwa amejiunga na klabu aliyoishabikia akiwa mtoto. Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na Arsenal ilikwisha mwisho wa mwezi Juni. Najihisi mtu maalum . Wengi wanajua kwamba nimekuwa na uhusiano mkubwa na klabu hii wakati wote nilipokuwa mtoto nikiwatizama wakicheza katika uwanja wa Upton Park Klabu hiyo pia inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Ukraine Andriy Yarmolenko. Tayari dau la yuro milioni 20 limekubaliwa na klabu ya Ujerumani Borussia Dortmund. Wilshere anatarajiwa kujiunga na kikosi cha mkufunzi mpya wa klabu hiyo Manuel Pellegrini nchini Switzerland ambapo klabu hiyo imekita kambi ikifanya mazoezi. Wakati huohuo kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira na mchezaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 Matteo Guendouzi wanatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu katika uwanja wa Emirates. The Gunners wameweka makubaliano n...

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 10.07.2018

Beki wa zamani wa Real Madrid Michel Salgado anaamini mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 24, ndiye anayelengwa na klabu hiyo msimu huu baada ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 26. (Talksport) Chelsea inajaribu kuipiku Manchester City katika kumsaini kiungo wa kati wa Lazio na Itali Jorginho, 26. (Manchester Evening News) City pia imembishia hodi kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Mateo Kovacic, 24, huku wakiwa na wasiwasi kuhusu kumtia mkobani Jorginho. (Mirror) Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 29, anatarajiwa kusalia na klabu hiyo licha ya kuhusishwa na uhamisho (Bild) Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Roma Monchi anasema kuwa ataangazia maombi ya kumuuza kipa wa Brazil Alisson lakini kufikia sasa hakuna klabu iliowasilisha ombi la kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (FourFourTwo) Manchester United na Real Madrid wamekutana na maafisa kutoka Lazio kujadili uhamisho wa kiungo wa...

Mtoto wa miaka miwili afariki baada ya kujipiga risasi Texas, Marekani

Christopher Williams Jr na babake Mtoto wa umri wa miaka miwili nchini Marekani amefariki baada ya kujipiga risasi kichwani kwa bunduki ambayo imekuwa ikihifadhiwa na wazazi wake nyumbani kwao. Polisi wa Houston, Texas wanasema wazazi wa mtoto huyo - Christopher Williams Jr - walikuwa nyumbani wakati wa kutokea kwa kisa hicho. Polisi wanasema bunduki hiyo ambayo hutumia risasi za ukubwa wa 9mm ilipatikana eneo la tukio na kwamba ilikuwa inamilikiwa na babake. Kufikia sasa, bado haijabainika iwapo wazazi wake watashtakiwa. Watoto kadha wamekuwa wakijipiga risasi na kujiua kimakosa nchini Marekani miaka ya karibuni. Polisi wa Houston wamesema wanajaribu kubaini ni vipi mtoto huyo aliyepewa jina la utani "Junior" aliweza kuifikia bunduki hiyo. Mkuu wa kitengo cha waathiriwa maalum katika idara ya polisi ya Houston David Angelo ametoa wito kwa wazazi walio na bunduki kuchukua tahadhari zaidi. "Ni lazima uweke salama silaha, iwe ni kwa kuhakiki...

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

SHERIA 17 ZA SOKA ======================= Mchezo wa soka ni moja ya michezo maarufu sana duniani na ni biashara kubwa sana katika ulimwengu wa michezo na ukitaka kuamini hili angalia makampuni yaliyowekeza katika kudhamini soka – ni makampuni makubwa makubwa yenye hadhi ya kitaifa na kimataifa. Kwa kuzingatia aina hii ya wadhamini, waendeshaji wa mchezo wa soka, wameweka kanuni na miongozo ya kufuatwa ili kuhakikisha kuwa wale wanaowekeza pesa zao wanaona thamani ya uwekezaji wao. Kwa hiyo soka kama ilivyo katika michezo mingine inazo kanuni na tutajadili kanuni moja baada ya nyingine kama zilivobainishwa katika muongozo wa FIFA unaojulikana kwa jina la Law of the Game. Sheria Namba 1: Dimba ============== NYASI - Dimba la soka litakuwa la nyasi asilia au bandia kulingana na kanuni za masindano na nyasi hizo lazima ziwe za rangi ya kijani. Kwa dimba la nyasi bandia na kama mchezo unaochezwa utakuwa wa kutambuliwa na FIFA, basi nyasi hizo bandia lazima zikidhi viwango maalumu ...

Boeing 787-8 Dreamliner: Mambo matano makuu aliyoyasema Magufuli kuhusu ndege mpya ya Tanzania

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli Jumapili aliongoza taifa hilo kupokea ndege mpya ya kisasa ambayo imenunuliwa kwa ajili ya kutumiwa na shirika la ndege la taifa hilo. Ndege hiyo mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ilinunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Taifa (ATCL). Bei ya ndege hiyo inakadiriwa kuwa $224.6 milioni (Sh512 bilioni za Tanzania) kwa mujibu wa taarifa kwenye tovuti ya kampuni ya Boeing. Ndege hiyo iliwasili majira ya saa 11:10 jioni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kisha kupewa heshima ya kumwagiwa maji na baadaye Rais Magufuli akiwa na viongozi wakuu walioambatana naye akaizindua rasmi. Aidha, yeye na Makamu wake Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, waliikagua kwa kuingia ndani ya ndege ili kujionea mandhari ya ndani. Mataifa ya Afrika yaliyo na Dreamliner Ethiopia (Ethiopian Airlines )*- 19 Kenya (Kenya Airways) - 8 Morocco ...