Mchezaji wa zamani wa Arsenal Jack Wilshere amejiunga na klabu ya West Ham kwa mkataba wa miaka mitatu na kusema kuwa amejiunga na klabu aliyoishabikia akiwa mtoto.
Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na Arsenal ilikwisha mwisho wa mwezi Juni.
Najihisi mtu maalum . Wengi wanajua kwamba nimekuwa na uhusiano mkubwa na klabu hii wakati wote nilipokuwa mtoto nikiwatizama wakicheza katika uwanja wa Upton Park
Klabu hiyo pia inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Ukraine Andriy Yarmolenko. Tayari dau la yuro milioni 20 limekubaliwa na klabu ya Ujerumani Borussia Dortmund.
Wilshere anatarajiwa kujiunga na kikosi cha mkufunzi mpya wa klabu hiyo Manuel Pellegrini nchini Switzerland ambapo klabu hiyo imekita kambi ikifanya mazoezi.
Wakati huohuo kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira na mchezaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 Matteo Guendouzi wanatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu katika uwanja wa Emirates.
The Gunners wameweka makubaliano na klabu ya Serie A Sampdoria kwa uhaimisho wa Torreira mwenye umri wa miaka 22 kwa dau la £26m .
Anaonekana kuwa mchezaji muhimu wa mkufunzi mpya Unai Emery ambaye tayari amewasajili wachezaji watatu.
Kiungo wa kati Guendouzi, 19, atajiunga na klabu hiyo kutoka Lorient na anaonekana mchezaji mahiri wa siku zijazo.
Makubaliano ya Torreira ambaye ana urefu wa futi 5 nchi 6 na ameichezea Uruguay mara nane yaliafikiwa kabla ya kombe la dunia, ambapo aliisaidia timu yake kufika robo fainali ambapo walilazwa 2-0 na Ufaransa.
Arsenal pia imemsajili beki wa Switzerland Stephan Lichtsteiner katika uhamisho huru kutoka mabingwa wa Itali Juventus, huku kipa wa Ujerumani Bernd Leno akikubali kujiunga na klabu hiyo kutoka Bayer Leverkusen.
Beki wa Ugiriki Sokratis Papastathopoulos amewasili Arsenal kutoka klabu ya ligi ya Bundesliga Borussia
Maoni