Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CHATU

Teknolojia mpya yatumika kumnasa chatu mkubwa mwenye mimba Florida, Marekani

NATIONAL PARK SERVICE Hifadhi moja ya taifa Florida, Marekani imemnasa chatu mkubwa mwenye urefu wa futi 17 (mita 5.2) kwa kutumia teknolojia mpya ya kuwanasa viumbe wavamizi. Nyoka jike huyo, ambaye ndiye mkubwa zaidi kuwahi kunaswa kwenye hifadhi ya Big Cypress alikuwa na uzito wa kilo 63.5 na alikuwa na 'mimba' ya mayai 73. Chatu ambao ni wavamizi kwenye eneo hilo wanatishia pakubwa maisha ya viumbe wa asili wa jimbo la Florida. Watafiti katika hifadhi hiyo waliwategeshea vifaa maalum madume ya chatu ili kuwatafuta majike yanayopandwa na kukaribia kutaga. "Timu ya watafiti ilimfuatilia dume moja lililofungwa kifaa hicho na kumnasa jike huyo karibu yake," imeeleza taarifa ya hifadhi hiyo kupitia mtandao wa Facebook. Pamoja na kuondosha nyoka wavamizi, hifadhi hiyo inatumia matokeo ya tafiti zake ili kustadi tabia za nyoka na kutengeneza njia mpya za kukabiliana nao. Chatu wanachukuliwa kama viumbe wavamizi jimboni Florida toka walipoonekana kwa mara ya k...