MTEULE THE BEST Viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuanza mazungumzo ya maandalizi kuhusu uhusiano wa kanda hiyo na Uingereza baada ya Brexit, licha ya kusisitiza kwamba hakuna hatua muhimu zilizopigwa katika mazungumzo. Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk alisema katika ujumbe wa Twita kuwa viongozi 27 wa kanda hiyo waliokutana mjini Brussels walikubaliana kuanzisha maadalizi ya mazungumzo ya biashara, baada ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel kusema hapo awali kwamba licha ya ucheleweshaji katika mazungumzo, kuna matumaini ya kufanikisha makubaliano ya mwisho. Taarifa ya maandishi ilioidhinishwa na viongozi hao ilisema Umoja wa Ulaya utachelewesha uamuzi juu ya kuanzisha hatua nyingine ya mazungumzo hadi mkutano ujao wa kilele mwezi Desemba, lakini walikubaliana kuanzisha majadiliano ya ndani ya maandalizi kuhusu biashara na uwezekano wa makubaliano ya mpito. Kasi ndogo ya mazungumzo, hasa kuhusu wajibu wa kifedha wa Uingereza, ilichochea hofu kwamba nchi...