Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Viongozi EU waidhinisha mazungumzo ya maandalizi Brexit

MTEULE THE BEST
Viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuanza mazungumzo ya maandalizi kuhusu uhusiano wa kanda hiyo na Uingereza baada ya Brexit, licha ya kusisitiza kwamba hakuna hatua muhimu zilizopigwa katika mazungumzo.
Belgien EU-Gipfel Theresa May und Donald Tusk (Reuters/G. Vanden Wijngaert)
Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk alisema katika ujumbe wa Twita kuwa viongozi 27 wa kanda hiyo waliokutana mjini Brussels walikubaliana kuanzisha maadalizi ya mazungumzo ya biashara, baada ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel kusema hapo awali kwamba licha ya ucheleweshaji katika mazungumzo, kuna matumaini ya kufanikisha makubaliano ya mwisho.
Taarifa ya maandishi ilioidhinishwa na viongozi hao ilisema Umoja wa Ulaya utachelewesha uamuzi juu ya kuanzisha hatua nyingine ya mazungumzo hadi mkutano ujao wa kilele mwezi Desemba, lakini walikubaliana kuanzisha majadiliano ya ndani ya maandalizi kuhusu biashara na uwezekano wa makubaliano ya mpito.
Kasi ndogo ya mazungumzo, hasa kuhusu wajibu wa kifedha wa Uingereza, ilichochea hofu kwamba nchi hiyo inaweza kuondoka Umoja wa Ulaya Machi 2019 bila makubaliano, na hivyo kuweka hatari ya sokomoko la kisheria na kiuchumi.
Belgien EU-Gipfel (Reuters/V. Mayo)
Wakuu wa mataifa na serikali za Umoja wa Ulaya wakiwa katika Mkutano wao wa kilele mjini Brussels Oktoba 20, 2017.
Merkel, kiongozi mwenye nguvu zaidi katika Umoja wa Ulaya, amesisitiza kuwa hakutaka hilo litokee, na kuogeza kuwa anachotaka ni makubaliano ya wazi na siyo tu suluhu isioyatabirika, akisisitiza lakini, kwamba Uingereza laazima itimize wajibu wake wa kifedha.
"Tunatumai kwamba kufikia Desemba tutakuwa tumepiga hatua za kutosha kuwezesha awamu ya pili kuanza lakini hiyo inategemea umbali gani Uingereza itakuwa imefikia ili tuweze kusema kwamba inatosheleza juu ya masuala makuu ya awamu ya kwanza," alisema Merkel na kuongeza kuwa, katika hayo suala la malipo ya fedha ndiyo muhimu zaidi.
'Hakuna muuzija'
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May aliungana na wenzake 27 kwa kifungua kinywa cha kikazi kuhusu mustakabali wa Umoja wa Ulaya, kabla ya kuondoka kuwapa nafasi ya kuzungumzia hali ya mazunguzo ya Brexit.
Umoja wa Ulaya unakubaliana kwamba kati ya masuala matatu makuu ya kutengana, suala la haki za raia ndiyo limepiga hatua lakini masuala yanayozusha ubishani zaidi yanaendelea kuwa malipo ya fedha za kujiondoa na mpaka wa Ireland ya Kaskazini na Ireland.
Rais wa Halmashuauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker, ambaye hapo awali alisema itakuwa muujiza kuendeleza mazungumzo hayo katika mkutano wa sasa, alisema Ijumaa kuwa haamini kwamba kutakuwepo na muujiza.
Duru kutoka Umoja wa Ulaya imesema kuanza kwa maandalizi kuhusu miongozo ya mazungumzo ya biashara kutaokoa muda ikiwa uamuzi wa kisiasa utachukuliwa kusonga mbele mwezi Desemba.
Belgien EU-Gipfel Jean-Claude Juncker (Reuters/D. Pignatelli)
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker anasema haoni muujiza ukitokea kuharakisha mazungumzo ya Brexit.
Uhusiano kati ya EU na Uturuki
Mkutano huo pia ulijadili juu ya uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki, ambapo viongozi wameiomba Halmashauri kuu kuzingatia njia ya kupunguza au kuhamisha fedha za ufadhili zilizopangiwa kutolewa kwa Uturuki kama sehemu ya maombi yake ya kuwa mwanachama wa umoja huo.
Umoja wa Ulaya uliahidi kuilipa Uturuki kiasi cha euro bilioni 4.45 kati ya mwaka 2014 na 2020 kama sehemu ya majadiliano ya kujiunga na umoja huo. fedha hizo zinalenga kuisaidia Uturuki kuboresha utawala wa sheria kulingana na vigezo vya umoja huo.
Mazungumzo juu ya kujiunga kwa Uturuki na Umoja wa Ulaya pamoja na kupanua umoja wa forodha kati ya EU na Uturuki yamekwama mnamo wakati uhusiano wa kidiplomasia unazidi kuwa baridi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...