Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Shinikizo laongezeka kwa viongozi wa jimbo la Catalonia

MTEULE THE BEST
Serikali ya Uhispania inajiandaa kutwaa mamlaka ya ndani ya utawala wa jimbo la Catalonia. Serikali hiyo kuu imepata uungwaji mkono kutoka kwa upinzani wa kulivunja bunge la Catalonia na pia kuandaa uchaguzi mpya.
Spanien Parlament in Barcelona Großkundgebung (Reuters/I. Alvarado)
Vyama vya kisiasa nchini Uhispania vinashinikiza kufanyike uchaguzi kwa sababu vinapendekeza kuwa hiyo ndio njia pekee ya kuinusuru nchi hiyo kutoka kwenye mgogoro mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini Uhispania katika kipindi cha miongo mingi. Chama cha upinzani cha Kisoshalisti kimesema kinaunga mkono hatua zozote zitakazochukuliwa na serikali kuu dhidi ya mamlaka ya jimbo la Catalonia ambalo kitisho chake cha kutaka kujitenga kimesababisha mtafaruku katika sarafu ya Euro ambao umeathiri hali ya uchumi wa jimbo hilo la nne kwa utajiri wa katika eneo la Umoja wa Ulaya. Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amesema utawala wa jimbo la Catalonia umekiuka sheria.
Spanien Premierminister Mariano Rajoy (Reuters/M. Vidal)
Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy
Waziri mkuu wa Uhispania Mriano Rajoy aliutaka upinzani ushirikiane naye ili aweze kuwasilisha msimamo wa pamoja dhidi serikali ya jimbo la Catalonia. Rajoy hapo kesho anatarajiwa kufanya mkutano maalum wa baraza la mawaziri ili kuuanzisha mchakato huo wa kuweka sheria ya lazima. Itakuwa ni mara ya kwanza tangu Uhispania kuingia katika demokrasia miongo minne iliyopita kuainisha ibara ya 155 ya katiba ya nchi hiyo inayoipa nguvu serikali kuu kuipokonya mamlaka serikali ya jimbo na kuitisha uchaguzi mpya. Waziri mkuu anataka aungwe mkono kwa kiwango kikubwa kabla ya kuichukua hatua hiyo ambayo imeongeza wasiwasi juu ya uwezekano wa kutokea maandamano makubwa katika jimbo la Catalonia.
Wateja wa benki
Wakati mgogoro wa kisiasa ukiendelea nchini Uhispania wateja wa mabenki wanaendelea kutoa fedha zao kwenye benki ambazo zimehamisha makao yao makuu na kuyapeleka katika sehemu zingine nchini Uhispania. Leo hii wateja wengi walionekana wakiwa wamepanga foleni ndefu wakisubiri kutoa fedha.  Benki za CaixaBank na Banco Sabadel ambazo ndio wakopeshaji wakubwa katika jimbo la Catalonia ni miongoni mwa taasisi za kifedha zilizohamisha biashara zao kutoka katika jimbo hilo la Catalonia. Kiongozi wa jimbo la Catalonia Carles Puigdemont ameshikilia msimamo wake bado anasema iwapo hakutakuwepo na mazungumzo baina ya upande wake na serikali atatangaza uhuru wa jimbo lake hilo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...