Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 15.10.2017

MTEULE THE BEST

Real Madrid wamewaambia Manchester United kuwa ikiwa wanahitaji kumsaini Gareth Bale 28, watalazimika kumuachia kipa David de Gea 26, ili ahamie Bernabeu. (Mirror)
Meneja wa zamani wa Livepool Rafa Benitez huenda akahama Newcastle kujiunga na Everton ikiwa Ronald Koeman ataihama Everton. (The Sun)
Mesut Ozil 28, na Alexis Sanchez wote wa Arsenal hawatakuwa na mikataba miwishoni mwa msimu na Arsenal inatakata kuwauza mwezi Januari. (Star)
Itawalazimu Liverpool na Barcelona kumng'ang'ania mlinzi wa Southampton Virgil van Dijik, ikiwa wangependa kumsaini mwezi Januari. (Mirror)
Everton wako tayari kutoa ofa ya pauni milioni 31 kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Sporting Lisbon, William Carvalho 25, licha ya klabu hiyo ya Ureno kusema kuwa haumuuzi. (Daily Mail, via Record)
Mshambuliaji wa Everton Henry Onyekuru 20, amethibitisha kuwa alikutana na maafisa wa klabu yake wiki iliyopita kuzungumzia kurejea mapema kutoka kwa mkopo na klabu ya Anderlecht. (Liverpool Echo)
Arsenal na Tottenham wote wanataka kumsaini wing'a wa Leicester Riyad Mahrez 26. (Mirror)
Mshambuliaji wa Torino Andrea Belotti 23, ambye analengwa na Manchester United na Chelsea atapewa mkataba mpya na klabu hiyo ya Italia. (Daily Mail, via Tuttosport)
Jevuntus wako mbioni na klabu ya nyingine ya Serie A ,Napoli kumsaini mlinzi wa Porto Diogo Dalot 18. (Mediagol - in Italian)
Real Madrid wanamawawinda wachezaji kadhaa wanaocheza kombe la dunia la wachezaji walio chini ya miaka 17, huku mshambuliaji Amine Gouiri akiwa nambari moja katika orodha yao. (Marca)
Meneja wa Manchster United Jose Mourinho alikataa ofa kutoka Liverpool ya kutaka awe meneja wao wakati akiwa meneja wa Chelsea. (Yahoo Sport)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...