Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya BOT

TANZANIA YAIKOSOA BENKI YA DUNIA

Ni kwanini Tanzania imekosoa makadirio ya benki ya dunia ya ukuaji wa uchumi wake Albina Chuwa, mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) Taasisi ya takwimu nchini Tanzania imesema kuwa inaweza kutathmini takwimu za ukuaji wa uchumi wake wa mwaka 2018 baada ya Benki ya dunia kutoa takwimu zilizoonyesha kiwango cha chini cha ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo. Waziri wa fedha wa Tanzania aliliambia bunge mwezi uliopita kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kilikuwa ni 7% mwaka jana. Benki ya dunia ambayo ilitoa hesabu zake kwa misingi ya data za taifa , matarajio ya mwaka 2019 ya ukuaji wa kiwango cha 5.4% - pia ilitoa kiwango cha chini cha ukuaji chini ya kile kilichokuwa kimekadiriwa na na serikali cha 7.1%. Albina Chuwa, mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ametetea njia zake na namna alivyofikia kiwango hicho, Reuters linaripoti. "Tumekwenda kote nchini kukusanya data halisi , sio sawa na mtu ambaye anakaa Washington na kutengeneza sampuli za pato la ndani ...