Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 12, 2016

Muuaji wa Jo Cox ajigamba mahakamani

MTEULE THE BEST   Muuaji wa Jo Cox ajigamba mahakamani   Thomas Mair, mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji ya mbunge wa Uingereza amefikishwa mahakamani Central London. Alipoambiwa aseme jina lake, mtu huyo mwenye umri wa miaka hamsini na mbili alisema nikimnukuu ''jina langu ni kifo kwa wasaliti,uhuru kwa Uingereza''. Mair pia ameshtakiwa kwa kumdhuru vibaya Cox,kupatikana na bunduki na silaha nyingine hatari.   Marehemu Jo Cox Marehemu Cox aliyekuwa akiwakilisha chama cha upinzani cha leba alipigwa risasi na kudungwa kisu katika eneo lake la uakilishi siku ya alhamisi. Kifo chake kimesababisha kusitishwa kwa majuma kadhaa kampeini za kura ya maoini juu ya Uingereza kujiondoa katika uanachama wa muungano wa EU  

Auawa akiwa katika facebook

MTEULE THE BEST     Auawa akiwa katika facebook live-stream     mtu mmoja nchini Chicago alipigwa risasi akiwa katika video ya moja kwa moja inayojulikana kama Live_stream katika mtandao wa Facebook ,polisi wamesema. Antonio Perkins mwenye umri wa miaka 28 alipigwa risasi katika kichwa na shingo magharibi mwa mji huo. Kanda hiyo ya video bado iko katika facebook na imeangaliwa mara 700,000. Ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu mjini Chicago ambapo mauaji yamefanyika moja kwa moja katika mtandao wa facebook. Mnamo mwezi Machi mtu asiyejulikana alipigwa risasi mara 16 wakati akipeperusha matangazo hewani. Hakuna mtu aliyekamatwa kufika sasa.Programu ya live-streaming ya facebook inawaruhusu watu kutangaza moja kwa moja mtandaoni .  

Auawa akichuma kuvu yenye 'nguvu za kiume'

MTEULE THE BEST       Mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa katika kijiji cha Nepal alipokuwa akichuma kuvu fulani inayotambuliwa kwa uwezo wake wa kuongeza nguvu za kiume. Kuvu hiyo inayotambulika kama ''Himalayan Viagra'' inasemekana kuwaongezea ashki walaji wake. Kuvu hiyo ni kitega uchumi cha wenye vijiji wa maeneo ya milimani. Haijulikani kwanini genge hilo la wavamizi liliwashambulia watu hao waliokuwa wakichuma kuvu hiyo katika wilaya ya mugu ila maafisa wa utawala wamethibitisha kuwa watu wengine watatu walijeruhiwa katika shambulizi hilo. Ukungu au kuvu hiyo humea kwenye mwili wa nondo au mtoto wa kipepeo na kilo moja ya kuvu hiyo inaweza kuuza kwa maelfu ya dola za Marekani nchini Uchina.   Auawa akichuma kuvu yenye 'nguvu za kiume' ...

Mohammed Morsi ahukumiwa kifungo cha maisha

MTEULE THE BEST     Mohammed Morsi ahukumiwa kifungo cha maisha     Mahakama ya Misri imempatia kifungo cha maisha jela aliyekuwa rais wa Kiislamu Mohammed Morsi baada ya kukamilika kwa kesi yake ya upelelezi. Ni miongoni mwa washtakiwa wanaoshtumiwa kwa kutoa nakala za siri kwa taifa la Qatar. Wakili wa Bw Morsi amesema kuwa aliwachiliwa huru kwa upelelezi lakini akapewa hukumu hiyo kutokana na kuliongoza kundi haramu. Wengine ni waandishi wawili wa Aljazeera ambao walihukumiwa kifo wakiwa hawako mahakamani.                             Aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi Hatahivyo kiongozi huyo wa zamani ana uwe...

KUMTUMAINIA MUNGU

MTEULE THE BEST TUMSIFU YESU KRISTO WAPENDWA KATIKA BWANA!!! MADA YA LEO: KUMTUMAINIA MUNGU SOMO; zaburi 11:1-7   Kwake MWENYEZI-MUNGU nakimbilia usalama; mnawezaje basi kuniambia "ruka kama ndege mpaka mlimani" Maana waovu wanavuta pinde wameweka mishale  tayari juu ya uta wawapige mshale watu wema gizani! Kama misingi ikiaribiwa mtu mwadilifu atafanya nini? MWENYEZI-MUNGU yumo hekaluni mwake takatifu ; kiti cha enzi cha MWENYEZI-MUNGU kiko mbinguni  Kwa macho yake huwachungulia wanadamu  na kujua kila  kitu wanachofanya MWENYEZI-MUNGU hupima waadilifu na waovu  huwachukia kabisa  watu wakatili  Atawanyeshea waovu makaa ya moto na madini ya kiberti upepo wa hari ndiyo itakuwa adhabu yao  MWENYEZI-MUNGU ni mwadilifu na apenda uadilifu watu wanyoofu watakaa pamoja naye NENO LA BWANA Unaruhusiwa kuchangia funguka tupate maoni yako MUNGU AKUBARIKI  

Picha za utupu hupunguza hamu ya kufanya mapenzi

MTEULE THE BEST   Picha za utupu hupunguza hamu ya kufanya mapenzi Watoto wengi hupata njia ya kutazama picha za ngono mitandaoni wakiwa na umri mdogo, kwa mujibu wa utafiti. Karibu asilimia 53 ya watoto walio kati ya umri wa miaka 11 na 16 wametizama picha za ngono mitandaoni, wote wakiwa ni asilimia 94, ya walioona picha hizo wakiwa na umri wa miaka 14 kulingana na utafiti wa chuo cha Middlesex. Utafiti huo unasema kuwa vijana kama hao, wako kwenye hatari ya kupoteza hamu ya kushiriki mapenzi. Serikali inasema kuwa ili kuhakikisha kuwa watoto wako salama na masuala ya mitandao ni jukumu kubwa. Watafiti waliwahoji watoto 1,001 walio na umri kati ya miaka 11 na 16, na kugundua kuwa asilimia 65 ya wale walio na umri wa kati ya miaka 15-16, walikubali kuona picha za ngono sawa na asilimia 28 ya wale walio kati ya miaka 11 na 12.  

TANZANIA KUFANYA BIASHARA NA QATAR

MTEULE THE BEST   Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa taifa lake linakusudia kufanya biashara na jamhuri ya Qatar haswa katika sekta ya gesi na usafiri wa ndege. Rais Magufuli aliyasema hayo baada ya kukutana na balozi wa Qatar nchini Tanzania bwana Abdallah Jassim Al Maadadi. Aidha rais Magufuli alitangaza nia ya kufungua ubalozi wa Tanzania mjini Doha kwa lengo la ''kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na taifa hilo tajiri la ghuba. "Najua Qatar ina uzoefu katika maeneo hayo na sisi Tanzania tungependa tushirikiane nanyi kuwekeza na kubadilishana uzoefu ili fursa hizo zilete manufaa kwa pande zote mbili" amesema bw Magufuli. TZ yataka uzoefu wa Qatar sekta ya gesi Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa sahihi na mkurugenzi wa mawa...

Philadelphia na kodi ya vinywaji

MTEULE THE BEST   Katika mji wa Philadelphia nchini Marekani wameanza kutoza kodi ya vinywaji vyenye sukari na kaboni licha ya kuwepo kwa mamilioni ya kampeni zilizofanywa na kampuni za vinywaji baridi kutaka kufungwa. Meya wa demokrasia ya Philadelphia,Jim Kenney alisema kodi hiyo itatumika kwenye maendeleo ya elimu na maeneo ya kupumzikia. Wakili wa afya wanasema vinywaji vyenye sukari vinasababisha watu kuongezeka uzito kupita kiasi na ugonjwa wa kisukari. Kodi hiyo imekosolewa vikali na wananchi wenye hali ya chini .Philadelphia ni mji wa pili baada ya mji wa Berkeley uliopo California kufanikiwa kuanzisha kutoza kodi ya aina hii.  

Mkewe Obama amtambua mbunifu kutoka Kenya

MTEULE THE BEST   Mkewe rais wa Marekani Michelle Obama amemsifu mjasiria mali kutoka Kenya mwanzilishi wa kampuni inayotengeza biadhaa za watoto bi Wanjiru Waithaka Waweru. Katika dhifa ya jioni iliyoandaliwa kwa heshma ya wanawake bi Wanjiru Waithaka Waweru, ambaye ni mhandisi/Msanifu mijengo ambaye amegusa maisha ya wengi kwa njia yake ya kipekee ya ubunifu wake unaozingatia maslahi ya watoto. Shirika lake la FunKidz, lilitajwa kama moja ya kupigiwa mfano na kuigwa kote duniani.   bi Wanjiru Waithaka Waweru, ambaye ni mhandisi/Msanifu mijengo ambaye amegusa maisha ya wengi kwa njia yake ya kipekee ya ubunifu wake unaozingatia maslahi ya watoto. Funkidz ilikuwa moja kati ya mashirika yanayongozwa na wanawake 10,000 kutoka Afrika Mashariki, mataifa...

Henrique Alves ajiuzulu kwa kashfa

MTEULE THE BEST   Waziri wa utalii nchini Brazil,Henrique Alves amejiuzulu siku moja baada ya kushutumiwa kujihusisha katika kampeni zisizo halali za kujipatia fedha kutoka kwa wanyonyaji wakubwa wa rushwa wa taifa wa kampuni ya mafuta, Petrobras. Alves ni waziri wa tatu kujiuzulu katika wa utawala wa raisi Michel Temer ambaye yuko katika muhula wa serikali iliyojaa kashfa. Waziri Alves akiwa bado anazipinga tuhuma hizo. Jumatano ,mahakama kuu imetoa ushaidi kutoka kwa mmoja wa wakuu wa Pretrobas, Sergio Machado ambaye amewahusisha wanasiasa ishirini wenye majina makubwa akiwemo raisi Temer ambaye pia amepinga kuhusika kuwasaidia wanachama wa chama chake katika harakati hizo zisizo halali.  

MWANANCHI

MTEULE THE BEST     Habari Biashara Michezo Habari CCM yashauriwa kubadili katiba Afa maji wakati akitafuta simu Chadema, polisi kukutana kortini leo Dk Ulisubisya atoa somo kwa taasisi, asasi za kiraia Makala ...

Mwanajeshi awaua watu 8 kwenye kambi Uganda

MTEULE THE BEST     Jumla ya watu wanane wameuawa baada ya kupigwa risasi ndani ya kambi ya kijeshi ya Makindye mjini kampala nchini Uganda Msemaji wa jeshi la Uganda meja Edward Birungi, anasema kuwa mwanajeshi huyo anaripotiwa kutofautiana na mkewe. Anaripotiwa kuwa mlevu na alikuwa pia amevuta bangi akiwa kazini, ambapo alianza kufyatua risasi kiholela akimtafuta mkewe ambaye alifanikiwa kutoroka. Wanawake wanne akiwemo mwanajeshi waliuawa wakati wa kisa hicho. Wengiwe waliouawa ni pamoja na wake wa wanajeshi wengine, wakiwemo pia watoto watatu. Mwanajeshi hyuo naye aliuawa kwa kupigwa risasi.  

FURAHA YA KWELI

MTEULE THE BEST TUMSIFU YESU KRISTO WAPENDWA KATIKA BWANA!!! MADA YA LEO: FURAHA YA KWELI SOMO: ZABURI 1:1-6  Heri mtu asiyefuata shauri la waovu, asiyeshiriki njia za wenye dhambi; wala kujumuika na wenye dharau; Bali huifurahia sheria ya MWENYEZI-MUNGU, na kuitafakari mchana na usiku  Huyo nikama mti uliopandwa kando ya vijito, unaozaa matunda kwa wakati wake,na majani yake hayanyauki  kila afanyalo hufanikiwa. Lakini waovu sivyo walivyo wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kwahiyo watu waovu wataanguka wakati wa hukumu wenye dhambi hawatakaa na kusanyiko la waadilifu. Maana MWENYEZI-MUNGU huziongoza njia za waadilifu lakinni njia za waovu zitishia katika maangamizi NENO LA BWANA!!!   Ndg yangu yangu mpendwa katika kristo MUNGU anakuonesha katika hili neno njia bora na sahihi nakuomba tuifuate njia ya KWELI NA UZIMA=YESU KRISTO  AHSANTE SANA UBARIKIWE  YESU ANAKUITA WEWE!!!!!!!

Mbunge wa chama cha Leba nchini Ungereza

MTEULE THE BEST    Mbunge wa chama cha Leba nchini Ungereza   Mbunge wa chama cha Leba nchini Ungereza Jo Cox ameaga dunia baada ya kupigwa risasi na kuchomwa kisu akiwa kwenye mkutano katika eneo lake la ubunge kaskazini mwa uingereza. Cox Ndiye mbunge wa kwanza kuuawa nchini Uingereza tangu Ian Gow auawe mwaka 1990. Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 52 aliyetajwa na majirani kama mtu asiye na marafiki amekamatwa na silaha kupatikana. Walioshuhudia wanasema kuwa mbunge huyo aliingilia kati mzozo kati ya wanaume wawili eneo ambapo alikuwa akikutana na watu eneo lake la ubunge. Mtu mmoja aliyeshuhudia alisema risasi ilifyatuliwa wakati Bi Cox aliingilia kati. Kisha muuaji akaanza kumchoma kisu alipokuwa amelala chini.  

Maisha ya Muhammad Ali

MTEULE THE BEST   Huu hapa ni mkusanyiko wa picha zinazosimulia matukio muhimu katika maisha ya Muhammad Ali, bingwa wa ndondi na mwanamichezo mashuhuri. Other Muhammad Ali alizaliwa na kupewa jina Cassius Marcellus Clay mjini Louisville, kentucky mnamo 17 Januari 1942. Alianza kucheza ndondi akiwa na umri wa miaka 12 na baadaye akaishia kushinda dhahabu katika uzani wa light-heavyweight Michezo ya Olimpiki ya Roma mwaka 1960. Other Ali alianza kucheza ndondi ya kulipwa Oktoba 1960 akiwa na umri wa miaka 18 na akashinda mara 18 mfululizo kabla ya kusafiri kwenda London Juni 1963 kwa pambano lake la kwanza la kulipwa ng'ambo. Alibashiri kwamba angemshinda bingwa wa Uingereza henry Cooper kupitia knockout raundi ya tano. ...