MTEULE THE BEST
waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko, anasema kuwa anaelewa kuwa huenda taifa lake likapigwa faini na shirikisho la soka la bara ulaya kutokana na tabia isiyofaa ya mashabiki wa timu ya taifa hilo.
UEFA, imeanza uchunguzi wa machafuko makali yaliyotokea baada ya mechi ya dimba la EURO kati ya Urusi na Uingereza katika mji wa Marseille nchini Ufaransa.Baada ya mechi kati ya mataifa hayo mawili, iliwabidi polisi kutumia gesi ya kutoa machozi pamoja na kunyunyuzia maji, ili kusitisha makabiliano hayo katika eneo la bandari mjini Marseille.
Kundi moja la mashabiki wa Urusi lilivuka kizingiti cha maafisa wa usalama na kuanza kuwashambulia mashabiki wa uingereza ndani ya uwanja.
Kulikuwa na makabiliano zaidi katika mji wa Nice kati ya mashabiki wa Ireland kaskazini na ufaransa ambapo watu sita walijeruhiwa.
Baadhi ya wanahabari wa uingereza wameelezea matukio hayo kwenye mitandao ya kijamii, na kunyooshea kidole cha lawama, genge la raia wa urusi waliovalia mavazi meusi, wakisema waliingia uwanjani wakiwa na nia ya kusababisha vurugu.
Maoni