MTEULE THE BEST
Polisi katika mji wa Orlando nchini marekani wanasema kuwa watu wengi wamepigwa risasi katika baa moja ya usiku.
Inaarifiwa kuwa takriban watu 20 wamejeruhiwa katika baa hiyo kwa jina Pulse, na kuwa mwanamme aliyejihami kwa bunduki aliwateka watu wengine.Polisi wanasema kuwa mshambuliaji huyo naye ameuawa. Vyombo vya habari nchini marekani vinaripoti vifo kadha.
Video iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa twitter, inaonyesha watu wakitibiwa nje ya baa hiyo, ambayo ni ya kwanza mjini humo kuwahudumia wapenzi wa jinsia moja.
Maoni