MTEULE THE BEST
Kikosi cha Misri kilichokuwa
kikitafuta mabaki ya ile ndege ya Egypt-Air iliyoanguka katika bahari ya
Mediterranea, kinasema kimepata kisanduku cheusi cha kuhifadhi
mawasiliano ya ndege.
Watafutaji hao wanasema kuwa, kifaa hicho kilikuwa kimeharibika, pale walipokipata chini ya sakafu ya bahari.Ndege hiyo ya EgyptAir chapa 804 muundo wa Airbus 320 na iliyokuwa ikitokea Paris, Ufaransa kuelekea Cairo, Misri, ilianguka na kuwauwa abiria wote 56 na wahudumu 10 waliokuwa ndani yake.