Kujikabidhi kwa Yule anayeongoza Kanisa
2025.05.08 Uchaguzi wa Papa wa ROma. (@Vatican Media) Mwariri mkuu wa Baraza la kipapa la Mawasiliano kwa mtazamo wa kuchaguliwa kwa Papa mpya ambaye amebainisha:“Leo hii ulimwengu uko katikati ya dhoruba,inayotikiswa na vita na jeuri.Tuombe amani.Tuombe pamoja na Petro na Petro ambaye leo hii alichukua jina la Leo,akiungana tena na Papa wa Waraka wa kitume wa “Rerum novarum.” Andrea Tornielli Jimbo la Roma lina Askofu wake, Kanisa la ulimwengu wote lina mchungaji wake. Kwa kasi ambayo inaweza kuwashangaza tu wale wanaosoma maisha ya Kanisa kupitia lenzi za siasa, Mkutano Mkuu umemteua Mrithi wa Petro. Asante, Baba Mtakatifu, kwa kukubali. Asante kwa kusema "ndiyo" na kwa kujiacha kwa Yeye anayeongoza Kanisa. Maneno ya kukumbukwa yaliyosemwa na Paulo VI mbele ya wanafunzi wa Chuo cha Lombardia , mnamo Desemba 1968, wakati wa kipindi kigumu cha kupinga katika kipindi cha baada ya mtaguso, yanakumbuka tena: “Wengi - alisema Papa - wanatarajia kutoka kwa Papa ishara za hisia, ...