Picha mpya za falaki yetu ya Milky Way
Mfumo wetu wa sayari na nyota, ama falaki, upo katika umbo la upinde na si nyoofu kama ilivyodhaniwa hapo awali, utafiti mpya umebaini.
Njia hiyo ya falaki, maarufu kwa lugha ya Kiingereza kama Milky Way, katika vitabu vyote vya sayansi na taaluma inaoneshwa ipo katika unyoofu.
Hata hivyo, utafifiti mpya wa nyota zing'aazo zaidi kwenye falaki hiyo umebaini kuwa nyota hizo hazipo kwenye njia nyoofu, zimepinda.
Wataalamu wa unajimu kutoka Chuo Kikuu cha Warsaw wanadhani kuwa nyota hizo zimepinda kutoka kwenye njia nyoofu ikiwa ni matokeo ya kutangamana na falaki nyengine za karibu.
Ramani mpya tatu za falaki ya Milky Wayzimechapishwa kwennye jarida la Science.
Picha maarufu zaidi ya Milky Way ikiwa katika mstari nyoofu imetokana na utafiti wa nyota milioni 2.5 kati ya nyota zipatazo bilioni 2.5 katika falaki hiyo. Dr University.
"Undani wa kimfumo na historia ya falaki ya Milky Way bado kabisa kujulikana, na moja ya sababu ni kuwa, ni vigumu sana kupima umbali baina ya nyota na maeneo mengine ya mbali ya falaki yetu," ameeleza Dkt Dorota Skowron kutoka Chuo Kikuu cha Warsaw.
Ili kupata picha ya kihalisia zaidi, Dkt Skowron na wataalamu wenzake walipima umbali wa baadhi ya nyota zing'aazo zaidi kwenye falaki yetu ya Milky Way. Nyota hizo ni kubwa, na za umri mdogo ambazo hung'aa mara elfu zaidi ya jua. Pia nyota hizo huongezeka ukubwa kwa kiwango cha juu kinachoendana na ung'aavu wake.
Hali hiyo ya ung'aavu na ukuaji wa nyota hizo unawawezesha wataalamu wa anga za mbali kukagua umali wao kwa ufanisi wa hali ya juu.
Nyingi ya nyota hizo ziligunduliwa kupitia kifaa kifahamikacho kama Optical Gravitational Lensing Experiment (OGLE) kilichopo kwenye eneo la Las Campanas, jangwa la Atacama nchini Chile.
Przemek Mroz, ambaye ni mjumbe wa timu ya OGLE amesema matokeo ya utafiti huo yanastaajabisha.
"Matokeo yetu yanaonesha kuwa falaki ya Milky Way Galaxy si nyoofu. Imepinda na kukunja kona kutoka kwenye kitovu chake. Kupinda huko kunaweza kuwa kumesababishwa na kutengamana na falaki nyengine ama kukutana na vitu vyeusi (vitu visivyoonekana lakini vipo ndani ya falaki)."
Matokeo hayo ya wataalamu kutoka Poland, yanaendana na matokeo mengine ya utafiti kuhusu nyota hizo ambayo yalichapishwa mwezi Februari na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Macquarie nchini Australia na Taasisi ya Sayansi ya Uchina
Maoni