Michael Job, mhubiri wa Marekani na muigizaji ambaye hivi majuzi alizuru Kenya na kuitwa 'Yesu bandia' hajafariki kama ilivyoangaziwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania na Kenya.
Kulingana na uchunguzi wetu jamaa huyo yupo hai na mzima wa afya.
Kadhalika, mhubiri huyo yupo nchini Kenya na kwamba hajatimuliwa kama ilivyodaiwa na vyombo hivyo vya habari.
Taarifa za vyombo hivyo ambazo zilianza kuenezwa siku tano zilizopita zinadai, Yesu huyo bandia alifariki siku chache tu baada ya kuhudhuria ibada ya kidini.
Mwisho wa ujumbe wa Facebook wa Michael
Inadaiwa kwamba alifariki siku chache tu baada ya kutembelea taifa hilo la Afrika mashariki baada ya kuuguwa ugonjwa wa mapafu.
Hata hivyo mhubiri huyo ameendelea kupakia mtandaoni picha na video ya shughuli zake siku baada ya siku.
Picha na video za karibuni zaidi alizipakia kwenye ukurasa wake wa Facebook saa nne usiku wa kuamkia leo.
Katika chapisho hilo na kanda za video alizoweka katika akaunti yake ya facebook Bwana Job anaonekana katika gari moja akihubiri Kiingereza huku akisaidiwa na mkalimani huku watu wakifuatilia mahubiri yake.
Aliandika: Leo mimi na Paul Maurer tulipata fursa ya kuhubiri juu ya gari la CFAN . mamia ya watu walifanya uamuzi wa yesu kuwa muokozi wa maisha yao. watoto wengi walimkaribisha Yesu na
Katika chapisho lake katika ukurasa wake wa facebook siku ya Jumatatu, muhuburi huyo aliandika: Ahsante Marc na Catrice mioyo yenu na utumishi wenu na Ahsanteni kwa kuja Kenya! Mungu aliwatumia ninyi kuokoa maisha ya watoto wengi. Kuhubiri Ukristo kwa masikini , kuwaponya wale waliovunjika moyo kuwaachilia waliotekwa, kuwafungulia waliokandamizwa, kuwaponya wengi na kuwaleta wengi karibu katika moyo wa Yesu. Ahsanteni kwa kanisa lenu na urafiki wenu. Waombeeni watu hawa wa Mungu! Tumsifu bwana! Nendeni duniani ili kuhubiri neno kwa viumbe vyote .Nenda ukahubiri injili kwa mtu hii leo. Mungu atakupatia ujasiri huu unavyozungumza . Anakusubiri. Ubarikiwe Ahsante kwa kutuombea!
Mwisho wa ujumbe 2 wa Facebook wa Michael
Mwisho wa ujumbe 3 wa Facebook wa Michael
Anaonekana akitangaza mkutano wa kidini utakaofanyika kuanzia Alhamisi wiki hii jijini Nakuru.
Picha za kanda za video zilizomuonyesha amevalia kama Yesu Kristo zilisambazwa katika mitandao ya kijamii kote barani Afrika.
Lakini jamaa huyu ni nani haswa na anafanya nini?
Mwanamume huyo ni mhubiri kutoka Marekani na muigizaji anayeitwa Michael Job, aliyekuwa anahudhuria misa ya madhehebu mbalimbali ya kikristo ambako alialikwa kuzungumza.
Anaishi Orlando, Florida, ambako amekuwa akiigiza kuwa Yesu katika bustani maalum The Holy Land Experience theme park, inayojitambulisha kama "jumba halisi la biblia la ukumbusho".
Watu wamekuwa wakifanya mzaha katika mtandao wa Twitter kuhusu picha zake na namna wachungaji barani Afrika wanapenda kudai kufanya miujiza.
Hii sio ziara yake ya kwanza barani Afrika, mapema mwaka huu alikuwa nchini Togo, licha ya kwamba picha alizoweka kutoka huko hakuonekana akiwa amevaa mavazi ya kuiga - bali alikuwa amevaa suti.
Alizuru pia Nigeria
Maoni