Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi












Neymar ameifungia PSG mabao 23 katika mechi 28 msimu huu

Real Madrid imeanza mazungumzo na Paris Saint-Germain kuhusu mpango wa kumsajili mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 27. (Sky Sports)



Azma ya Barcelona kumsajili tena Neymar, 27, inategemea ikiwa klabu hiyo itamuuza Philippe Coutinho ambaye pia ni mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Brazil. (Goal)

Manchester United wako tayari kulipa Ā£81m ambayo itawawezesha kumnyakua mshambuliaji wa Uhispania na Athletic Bilbao Inaki Williams, 25. (El Chiringuito TV - via Mail)


Pendekezo la Leroy Sane kuhamia Bayern Munich kutoka Manchester City limeathiriwa na jeraha la goti linalomkabili nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Mail)


Leroy Sane (Kulia)

Beki wa Chelsea Mbrazil David Luiz, 32, ataruhusiwa kujiunga na Arsenal kwa Ā£8m tu. (Mirror)

Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha,26, amewasilisha ombi la kutaka uhamisho huku kukiwa na tetesi kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast akipingiwa upatu kuhamia Everton. (Express)

Palace wameiambia Everton hawatakubali kupokea chini Ā£100m kumwachilia mshambuliaji huyof. (Guardian)



Everton wanatarajiwa kuwasajili beki waChelsea na kiungo wa kimataifa wa England wa wachezaji wa chinii ya miaka 21 Fikayo Tomori, 21, na beki wa kati wa Bournemouth Mholanzi Nathan Ake, 24. (Sun)

Newcastle wanakaribia kumsajili beki wa kulia - na nyuma Mswidi Emil Krafth, 25, kutoka klabu ya Ufaransa ya Amiens. (Newcastle Chronicle)

Burnley wamewasilisha ombi la dakika ya mwisho kumsaini kiungo wa kati Danny Drinkwater, 29, kwa mkopo kutoka Chelsea. (Mail)



Tottenham wanakaribia pia kumsaini bekki wa kushoto wa Fulham Ryan Sessegnon, 19. (Mirror)

Atletico Madrid wanajiandaa kumsajili mchezajiwa safu ya kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Independent)

Kingo wa kati wa Juventus Sami Khedira, 32, amekataa uwezekano wa uhamisho mara mbili kwa sababu anaazimia kujiunga na Arsenal. (Star)


Sami Khedira, kiungo wa kati wa Juventus

Wolves wamesitisha mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 25. (Express & Star - via Daily Echo)

Robert Lewandowski ametoa wito kwa Bayern Munich kuwasajili wachezaji watatu wapya.

Mshambuliaji huyo wa Poland anataka kuimarishwa kwa safu ya mashambulizi baada ya wachezaji nyota kuhama klabu hiyo. (Goal)


Robert Lewandowski


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...