Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TALAKA L

Siku hizi talaka zimezidi - Askofu Malasusa

Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa amedai kuwa kwa sasa jamii imekosa hali ya upendo hali inayosababisha kuongezeka kwa matukio ya mahusiano mengi kuvunjika. Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa. Askofu Malasusa amesema kauli hiyo Desemba 25, 2018  katika ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam ambapo amesema wana ndoa wengi wanahofu na mahusiano. Malasusa amesema “siku hizi talaka zimezidi jamii haina upendo wala hofu ya Mungu, hofu imejaa katika ulimwengu, wengi waliopo katika ndoa hawana hakika kama wataendelea,’’ amesema. Aidha ameongeza kuwa “malaika anasema usiogope nitawaletea habari njema, tena katika aya yetu ya siku ya leo tunasema tumepewa mtoto mwanamume, yeye yupo tayari kubadilisha mitazamo yetu kutuondoa katika hofu na kuwa wajasiri katika maisha yetu....