Jambazi sugu ametoroka jela kwa kutumia ndege aina ya helikopta katika jela moja mjini Paris , mamlaka ya Paris imesema. Redoine Faid alisaidiwa na watu kadhaa waliojihami ambao walitengeneza mwanya katika lango la jela hiyo huku helikopta hiyo ikitua katika uwanja karibu na jela hiyo. Ndege hiyo ilipaa hadi eneo la Gonessa lililopo karibu na jela hiyo ambapo ilipatikana na maafisa wa polisi. Faid 46, amekuwa akihudumia kifungo cha miaka 25 kwa jaribio la wizi wa mabavu lililotibuka ambapo afisa mmoja wa polisi aliuawa. Hii ni mara yake ya pili kutoroka jela: Mwaka 2013 alitoroka jela baada ya kuwatumia walinzi wanne kama ngao huku akilipua milango kadhaa kwa kutumia kilipuzi. Alifanikiwa kutoroka chini ya nusu saa baada ya kuwasili katika jela hiyo iliopo kaskazini mwa Ufaransa. Mwaka 2009 Faid aliandika kitabu kuhusu uzoefu wake katika mitaa ya Paris iliojaa uhalifu na kuwa mtu aliyekukuwa akivunja sheria mara kwa mara. Alidai kuwacha uhalifu lakini mwaka mmoja baad...