Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya WAZIRI

MAPACHA WATANZANIA WALIOUNGANA WATENGANISHWA

  MAPACHA wa Tanzania walioungana, Anishia na Melanese, wametenganishwa nchini Saudi Arabia Desemba 23, 2018, na hali zao zinaendelea vizuri kwa wakati huu.   Jumanne Desemba 25, 2018 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Aminiel Aligaesha amethibitisha mapacha hao kutenganishwa.   Kwa mujibu wa gazeti la nchini Saudi Arabia, saudigazette.com mapacha hao walitenganishwa na jopo la wataalamu 32 kwa muda wa saa 13.   Upasuaji huo uliofanyika katika hospitali ya Mfalme Abdullah, (King Abdullah Children’s Specialist Hospital) iliyopo katika mji wa Riyadh (King Abdulaziz Medical City), uliongozwa na Dk Abdullah Al-Rabeeah.   Mapacha hao wa kike waliozaliwa katika Kituo cha Afya cha Missenyi, Kagera, Januari 2018,  walipofikishwa Saudi Arabia walifanyiwa vipimo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vya kuona uwezekano wa kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha

Mizengo Pinda azungumzia Upinzani

Mizengo Pinda azungumzia maumivu ya Upinzani Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ameweka wazi jinsi alivyokuwa akiumizwa na kauli za upinzani dhidi ya uongozi wake na kusema kuwa anaushangaa upinzani kulalamikia uongozi ambao waliulilia kwa muda mrefu. Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda. Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma, Pinda amesema kuna kipindi wakati wa uongozi wake, wapinzani walikuwa wakiinyooshea kidole serikali yao kuwa ni dhaifu haina makali, hivyo walikuwa wanataka kiongozi mkali na mwenye uamuzi mgumu. " Kauli hiyo na ilikuwa ikinikera kwa sababu ilitulenga viongozi wa wakati ule, lakini sasa nashangaa kuona wapinzani haohao wameanza kulalamika tena juu ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli ambaye ndiye kiongozi wa aina waliyekuwa wakitamani kumpata" , amesema Pinda. Pinda amesema kuwa, Rais Magufuli ndiye kiongozi ambaye Watanzania walikuwa wanamhitaji kutokana na uthubutu alionao katika kutekeleza miradi ...

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda Wasanii kutumia mitandao kutangaza utalii

Picha za Amber Rutty zinaleta joto DSM" - Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wasanii kutumia mitandao ya Kijamii kuhamasisha masuala ya Utalii wa nchi ili waweze kuitangaza Tanzania kupitia wafuasi wao wa mitandao ya kijamii ambao wanapatikana nchi mbalimbali. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia), na Amber Rutty. Akizungumza Jijini Dar es salaam, mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na Waziri Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla, Makonda amewataka wasanii wapewe nafasi ya kutangaza utalii huo. Makonda amesema " niwaombe wananchi wa Dar es salaam tutumie fursa hii kutangaza utalii wetu, niwaombe wasanii wenye wafuasi mitandaoni watangaze utalii wetu hapa nchini ili dunia ifahamu kuliko kusambaza picha za Amber Rutty ambazo zinaleta joto kali na laana ". " Tunatamani Dar es salaam isiwe sehemu ya kupita bali iwe sehemu ya watu kukaa, kwa sababu tuna maeneo ya utalii, ikiwemo ghorofa la kwanza kujengwa Ta...