Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Zanzibar Tanzania

Azimio la Zanzibar 2018: Viongozi wa upinzani Tanzania waafikiana 'kudai demokrasia' kwa pamoja

iovngozi hao wameeleza mkutano huo wa Zanzibar kuwa wa kihistoria Vyama sita vya upinzani nchini Tanzania vimekutana na kutoa azimio la pamoja katika kile kinachotazamwa kama juhudi za mapema za kutaka kuungana nchini humo. Viongozi hao waliahidi kuungana na kuutangaza mwaka 2019 kuwa ni 'Mwaka wa Kudai Demokrasia', na kadhalika wakaahidi kufanya mikutano ya siasa bila kujali katazo la mikutano ya hadhara. "Ni mwaka ambao tutapambana kuzidai haki zetu zote tunazonyimwa kinyume na sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," taarifa ya pamoja ya viongozi wa vyama hivyo inasema. "Kama vyama vya siasa vyenye uhalali na vyenye utaratibu uliowekwa rasmi kisheria na kikatiba, tutatangaza rasmi namna na utaratibu wa kufanya mikutano yetu ya hadhara katika kila kona ya nchi yetu, hatutaruhusu katazo haramu na lisilo na mashiko ya kisheria litumike kutuzuia kutekeleza wajibu wetu." Waliotia saini azimio hilo ni Maalim Seif Sharif Hamad (Katibu Mkuu...

Tanzania yafafanua madai ya upotevu wa trilioni 1.5

Baada ya juma zima la kuwepo kwa hofu ya kutoweka kiasi cha shilingi trilioni 1.5 za Kitanzania serikalini, hatimaye leo serikali ya Rais John Magufuli imetoa ufafanuzi bungeni juu ya wapi kilipo kiasi hicho cha fedha. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli. Baada ya juma zima la kuwepo kwa hofu ya kutoweka kiasi cha shilingi trilioni 1.5 za Kitanzania katika mazingira ya kutatanisha katika makadirio ya bajeti ya serikali ya Tanzania, hatimaye leo serikali ya Rais John Magufuli imetoa ufafanuzi bungeni juu ya wapi kilipo kiasi hicho cha fedha. Ufafanuzi huu unatolewa baada ya kuwepo kwa kile kilichoonekana kama ukosoaji wa wazi na wasiwasi juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma na yasiozingatia sheria kutoka kwa viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani na hata wananchi wa kawaida kwa takribani juma zima. Akitoa mchanganuo wake, Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji amesema kiasi cha shilingi bilioni 697 kilitumika kwa matumizi ya dhamana...

Kwa Picha: Watu walivyoukaribisha Mwaka Mpya wa 2018 miji mbalimbali duniani

MTEULE THE BEST Watu duniani waukaribisha mwaka 2018 kwa Sherehe Watu kote duniani wameukaribisha mwaka mpya wa 2018 kwa sherehe mbali mbali zikiwemo kufyatua fataki na kushiriki ibada maalum. Miongoni mwa nchi zilizoukaribisha kwanza mwaka huu mpya ni Australia ambako fataki ziliwashwa katika jengo maarufu la Sydney Opera.Hapa Ujerumani sherehe za kuukaribisha mwaka mpya zilifanyika chini ya usalama mkali kuepusha matukio ya uvunjaji sheria kama ilivyoshudiwa miaka miwili iliyopita ambapo wanawake walinyanyaswa kingono katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya mjini Cologne. Polisi mjini Berlin iliongeza askari 1,600 wa kushika doria.Hii leo Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ataendesha misa katika ukumbi wa Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Vatican ambako atahimiza kuwepo amani duniani na kuhimiza ujumbe wa kuwajali wasiobahatika katika jamii hasa wahamiaji na wakimbizi. Ulimwengu unapoendelea kusherehekea kufika kwa mwaka mpya wa 2018, sherehe za aina yake z...