Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CAG

Ripoti ya CAG yawasilishwa Bungeni Tanzania, asisitiza neno dhaifu ni la kawaida

Prof Mussa Assad ametiwa hatiani na Bunge kwa tuhuma za kudharau chombo hicho. Mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania Prof Mussa Assad amesisitiza kuwa ataendelea kutumia neno dhaifu. Akiongea na waandishi wa habari baada ya ripoti zake kuwasilishwa Bungeni, Prof Assad amesema neno hilo ni la kawaida kwenye fani ya uhasibu. "Neno 'dhaifu' naendelea kusisitiza ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. Na tutaendelea kulitumia," Prof Assad amesema. Hata hivyo Prof Assad hakuwepo Bungeni kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Mkutano wake na wanahabari umefanyika kwenye ofisi yake mjini Dodoma. "Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma," amesema Prof Assad. Azam TV@azamtvtz “Kwa mwaka 2017 tulitoa mapendekezo 350, yaliyotekelezwa kwa ukamilifu ni mapendekezo 8...

RPC Gilles Muroto: Watakaoandamana Dodoma watapigwa hadi kuchakaa

Raia watakaondamana kwa lengo la kuwashinikiza wabunge kushirikiana na Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG nchini Tanzania watakiona cha mtema kuni. Onyo hilo limetoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto ambaye amewatahadharisha waliopanga maandamano hayo hapo siku ya Jumanne kwamba watapigwa hadi ''kuchakaa''. Afisa huyo amesema kwamba baadhi ya vyama vya upinzani ikiwemo ACT Wazalendo wamepanga kufanya maandamano kesho kulishinikiza Bunge kufuta kauli yake ya kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad. Muroto ameonya kuwa wale wanaopanaga kufanya safari kuelekea mjini Dodoma ili kushiriki katika maandamano hayo wataambulia kupigwa na kuchakaa. ''Wale wote waliopanga kufanya maandamano mnamo Aprili 9, 2019 wasije kuingia barabarani maana watapigwa na kuchakaa," amesema Muroto. Afisa huyo amesisitiza kuwa maswala ya bunge hutekelezwa ndani ya bunge na wala sio nje hivyoba...