Marekani kutekeleza adhabu kifo kwa mara ya kwanza tangu 2003 “Idara ya haki inazingatia utawala wa sheria kwa sababu tunawajibu wa kuitendea haki familia ya wahasiriwa wa mauaji ," anasema mwanasheria mkuu William Barr Serikali ya Marekani imeidhinisha adhabu ya kifo ianze tena kutekelezwa baada ya adhabu hiyo kusitishwa miaka 16 iliyopita, yasema Idara ya mahakama. Katika taarifa mwanasheria mkuu William Barr amesema kuwa tayari ameiiagiza Halmashauri ya magereza kupanga siku ya kunyongwa kwa wafungwa watano waliopewa adhabu hiyo. Bw. Barr amesema watano hao walishitakiwa kwa kuhusika na mauaji na ubakaji wa watoto na watu wazima. Hukumu dhidi yao imepangwa kutekelezwa Decemba 2019 na Januari 2020. "Kwa kuzingatia pande zote mbili husika, Idara ya haki imeomba kutekelezwa kwa hukumu ya kifo dhidi ya wahalifu sugu," ilisema tarifa ya Bw. Barr. "Idara ya haki inazingatia kikamilifu utawala wa sheria - na ni wajibu wake kutekeleza hukumu iliyotolewa d...