Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Serikali ya Marekani imeidhinisha adhabu ya kifo ianze tena

Marekani kutekeleza adhabu kifo kwa mara ya kwanza tangu 2003



“Idara ya haki inazingatia utawala wa sheria kwa sababu tunawajibu wa kuitendea haki familia ya wahasiriwa wa mauaji ," anasema mwanasheria mkuu William Barr

Serikali ya Marekani imeidhinisha adhabu ya kifo ianze tena kutekelezwa baada ya adhabu hiyo kusitishwa miaka 16 iliyopita, yasema Idara ya mahakama.


Katika taarifa mwanasheria mkuu William Barr amesema kuwa tayari ameiiagiza Halmashauri ya magereza kupanga siku ya kunyongwa kwa wafungwa watano waliopewa adhabu hiyo.

Bw. Barr amesema watano hao walishitakiwa kwa kuhusika na mauaji na ubakaji wa watoto na watu wazima.


Hukumu dhidi yao imepangwa kutekelezwa Decemba 2019 na Januari 2020.

"Kwa kuzingatia pande zote mbili husika, Idara ya haki imeomba kutekelezwa kwa hukumu ya kifo dhidi ya wahalifu sugu," ilisema tarifa ya Bw. Barr.

"Idara ya haki inazingatia kikamilifu utawala wa sheria - na ni wajibu wake kutekeleza hukumu iliyotolewa dhidi ya mshtakiwa kwa niaba ya wahasiriwa wa uhalifu na familia zao."

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionChumba cha mauaji, Huntsville, Texas

Tangazo hilo limefutilia mbali makubaliano ambayo hayakuwa rasmi ya kusitisha adhabu ya kifo - hali ambayo ilikuwa inapinga uamuzi wa mahakama kuhusu adhabu ya kifo.

Adhabu hiyo ilitekelezwa mara ya mwisho mwaka 2003 dhidi ya Louis Jones Jr, 53, mbabe wa vita vya Ghuba aliyemua askari wa miaka 19 Tracie Joy McBride.

Adhabu ya kifo iliondolewa na mamlaka ya majimbo nchini Marekani mwaka 1972 lakini uamuzi huo ulibatilishwa na mahakama bya juu zaidi mwaka 1988.

Kwa mujibu wa data zilizokusanywa na kituo kinachonakili taarifa kuhusu adhabu ya kifo, watu 78 walihukumiwa adhabu ya kifo kati ya mwaka 1988 na 2018 lakini ni watatu kati ya waliouawa.

Kuna wafungwa 62 ambao wanakabiliwa na hukumu ya kifo kufikia sasa.


Br. Barr amesema kuwa ameiagiza Halmashauri ya magereza kubuni sera itakayoidhinisha utumizi wa dawa moja kumuua mtu badala ya kutumia aina tatuya dawa ambayo ilikuwa ikitumika hapo mbeleni.

Mtu anapodungwa sindano ya sumu ya dawa hiyo anapatwa na usingizi, baadae viungo vyake vya mwili hulemaa pole pole hadi mfumo wa neva unapoacha kufanya kazi taratibu akiwa bado usingizini hadi umauti unapomfika.

Idara ya haki imesema watu watano walio kwenye orodha ya kifo ni:

Daniel Lee Lewis, aliyeua familia ya watu watatu akiwemo mtoto wa kike wa miaka minane.

Lezmond Mitchell, aliyemuua mwanamke wa miaka 63 na mjukuu wake wa mwaka mmoja.

Wesley Ira Purkey,aliyembaka na kumuua msichana wa miaka 16 na pia kumuua mwanamkea wa miaka 80.

Alfred Bourgeois, aliyemnyanyasa na kumuua mtoto wake mdogo wa kike wa miaka miwili.

Dustin Lee Honken, ambaye aliwaua watu watano miongoni mwao watoto wawili.

Mauaji ya watu hao yatafanyika katika Jela ya Terre Haute linalowazuilia wafungwa wanaokabiliwa na uhalifu mkubwa, mjini Indiana, mauaji ya wengine yatekelezwa baadae, idara ya haki ilisema.

Adhabu ya kifo Marekani

Adhabu ya kifo imehalalishwa kisheria katika majimbo 29 nchini Marekani


Tangu mwaka 1976, Jimbo la Texas limetekeleza adhabu (561),ikifuatiwa na Virginia (113) na Oklahoma (112)


Kuna wafungwa 2,673 wanaokabiliwa na hukumu ya kifo nchini Marekani


California inaidadi kubwa ya wafungwa waliohukumiwa kifo - 733 - lakini ni wafungwa 13 pekee waliouawa tangu mwaka 1976


Idadi ya kila mwaka ya hukumu ya kifo kwa imepungua kwa 85% kati ya mwaka 1998 na 2018 - kutoka 295 hadi 43


Chanzo: Taarifa ya Kituo cha adhabu ya kifo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...