Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za Soka Ulaya leo Ijumaa

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 26.07.2019: Zaha, Maguire, Bale, Pogba, Neymar, Malcom



Manchester United huenda ikalazimika kulipa Leicester City £80m kumnunua mlinzi wake Harry Maguire baada ya Eric Bailly kuumia goti katika mechi ya kirafiki dhidi ya Tottenham. (Mirror)


Winga wa Leicester Muingereza Demarai Gray 23- amesema hakuna haja ya kuwa na "hofu" kuhusu uhamisho wa Maguire na kuongeza kuwa haamini nyota huyo wa miaka, 26, ana msongo wa mawazo kuhusu hatma yake. (Leicester Mercury)


Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amepuuzilia mbali madai kuwa wanamlenga mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 30, na kusisitiza kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni kuimarisha kikosi kilichopo badala ya kununua wachezaji wapya. (Independent)


Gareth Bale alijiunga na Real Madrid mwaka 2013

Everton imeifahamisha Crystal Palace kuwa wanaandaa dao la £60m kumnunua mshambuliiaji wa Uturuki Cenk Tosun kama sehemu ya mkataba wa kumzuilia mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26 -lakini wanahofia huenda akanyakuliwa na Chelsea. (Telegraph)



Manchester United inajiandaa kumnunua mchezaji wa Lazio na nyota wa kimataifa wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic kare kwa kima cha £70m ,kuchukua nafasi ya kiungo wakati mfaransa Paul Pogba endapo ataamua kuhama klabu hiyo. (Mirror)


Ole Gunnar Solskjaer (kushoto) na Paul Pogba

Hata hivyo Kuna tetesi huenda, Pogba akasalia Old Trafford kwa mwaka mwingine mmoja, hatua ambayo huenda ikamnyima nafasi Milinkovic-Savic (Express)


Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, 34, hana uwezo wa kumshawishi Neymar kujiunga na miamba wa Italia- kwa sababu nyota huyo wa Brazil wa miaka 27-ameamua kujiunga na Barcelona. (Star)


Cristiano Ronaldo

Borussia Dortmund wanafanya mazungumzo ya kumsajili mshambulizi wa Barcelona Malcom kwa euro milioni 42 (£37.5m). (Goal)

Mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Moussa Dembele , 23, atakuwa katika urodha ya kujiunga na Manchester United klabu hiyo ikiamua kumuuza nyota wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26. (Sky Sports)


Thamani ya uhamisho wa mlinzi wa Spurs Toby Alderweireld imeongezeka mara dufu baada ya masharti ya mkataba wa £25m wa kumuachilia kiungo huyo raia wa Ubelgiji wa miaka 30 kufikia kikomo siku ya Alhamisi. (Sun)


Mlinzi wa Spurs Toby Alderweireld

Meneja wa Napoli Carlo Ancelotti ana matumaini klabu yake itamsajili mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 28, kutoka Real Madrid msimu huu. (Marca)



Manchester United huenda wakalazimika kutumia zaidi ya £30m kumpata kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff,21. (Manchester Evening News)

Tottenham imewasiliana na Juventus kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Argentina international mshambuliaji Paulo Dybala, 25, ambaye bei yake anayekadiriwa kuwa £80m. (Evening Standard)


Paolo Dybala

Aston Villa wanakaribia kukamilisha usajili wa mchezaji wa 11 kabla ya dirisha la uhamisho wa wachezaji kufungwa -tayari wametumia £120m - na wanatarajiwa kuilipa klabu ya Brugge £11 ili kumunua mchezaji wa kimataifa wa Zimbabwe Marvelous Nakamba, 25. (

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...