Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAGUFULI

PICHA| UZINDUZI WA KARAKANA YA KUU YA JESHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezindua karakana kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) - Lugalo jijini Dar es salaam. Machi 13, 2020

RAIS WA TANZANIA ATOA TAHADHARI KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORANA

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania, John Magufuli ametoa tahadhari kuhusu ugonjwa unaotokana na virusi vya corona, akiwataka kutopuuza kwani mpaka sasa umegharimu maisha ya watu wengi duniani. Amezungumza na Umma wa Tanzania alipokuwa akizindua karakana ya jeshi hii leo jijini Dar Es Salaam. Katika kusisitiza tahadhari iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa afya nchini humo, Ummy Mwalimu, Rais Magufuli amewataka raia kutopuuza tahadhari hizo. ''Ugonjwa upo na umekumba nchi nyingi kwa takwimu zilizopo ni kwamba zaidi ya watu 100,000 wameambukizwa na watu 4,500 wamepoteza maisha.'' ''Tunatambua kuwa Tanzania mpaka sasa hatuna mgonjwa wa corona lakini hatuwezi kujiweka pembeni bila kuchukua hatua na hatua zimeanza kuchukuliwa waziri wa wizara ya afya ameshatoa tahadhari tunazopaswa kuchukua''. ''Ugonjwa huu unaua na unaua kwa haraka, sana niwaombe tusipuuze, tusipuuze hata kidogo ni lazima kuchukua hatua za kujikinga...

Magazeti ya leo Ijumaa Julai 19 2019

 MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 19 2019  

Rais Magufuli apokea majina ya kuyakata mishahara

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Ladislaus Matindi, ameeleza tayari ameshamkabidhi Rais Magufuli orodha ya majina ya viongozi ambao walikatisha safari zao za ndege katika shirika hilo licha ya kukatiwa tiketi za serikali. Rais Magfuli Akizungumza Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi, amedai wameshatekeleza agizo hilo la Rais Magufuli ambalo alilitoa kwenye hafla ya upokeaji wa ndege mpya ya Tanzania A220-300 aina ya Airbus. Matindi amesema “ majina ya vigogo husika tumeshayakabidhi kwa Rais, tangu tumeelekezwa tulifanyia kazi maelekezo hayo na kisha tukayakabidhi sehemu husika ,” “ Siwezi kutaja ni vigogo wa kada gani, wasiliana na Ofisi ya Rais wataweza kuwa na majina pamoja na Idara au Taasisi wanazotoka, sisi tumepeleka orodha ,” ameongeza Luhindi. Akizungumza Desemba 23, 2018 Rais Magufuli alisema “nimeambiwa pia baadhi ya tiketi huwa zinakatwa na watendaji wa serikali halafu wakati wa mwisho haw...

Mizengo Pinda azungumzia Upinzani

Mizengo Pinda azungumzia maumivu ya Upinzani Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ameweka wazi jinsi alivyokuwa akiumizwa na kauli za upinzani dhidi ya uongozi wake na kusema kuwa anaushangaa upinzani kulalamikia uongozi ambao waliulilia kwa muda mrefu. Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda. Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma, Pinda amesema kuna kipindi wakati wa uongozi wake, wapinzani walikuwa wakiinyooshea kidole serikali yao kuwa ni dhaifu haina makali, hivyo walikuwa wanataka kiongozi mkali na mwenye uamuzi mgumu. " Kauli hiyo na ilikuwa ikinikera kwa sababu ilitulenga viongozi wa wakati ule, lakini sasa nashangaa kuona wapinzani haohao wameanza kulalamika tena juu ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli ambaye ndiye kiongozi wa aina waliyekuwa wakitamani kumpata" , amesema Pinda. Pinda amesema kuwa, Rais Magufuli ndiye kiongozi ambaye Watanzania walikuwa wanamhitaji kutokana na uthubutu alionao katika kutekeleza miradi ...

MAPUNDA: Azawadiwa kwa kuturosha ndege

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemkabidhi kiasi cha shilingi milioni 10, Mtanzania ambaye alisababisha Shirika la Ndege la Tanzania kuwa na ndege ya kwanza ambaye anafahamika kwa jina la Mapunda. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli. Rais Magufuli ametoa zawadi hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa mapokezi ya ndege ya kwanza Afrika aina ya Air Bus A220-300 ambapo alimpongeza Mzee Mapunda kwa kuhatarisha maisha yake pindi alipokuwa angani akirejea Tanzania baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika ambao ndio walikuwa wamiliki wa ndege hizo. Aidha katika mkutano huo Rais Magufuli alimuagiza Waziri wa Uchukuzi, Isaac Kamwelwe kuhakikisha Mapunda na mkewe wanasafiri bure kwenye ndege za ATCL katika safari zake zote. " Kikubwa ninawaomba watanzania tuwe wazalendo, Mapunda asingekuwa mzalendo leo tusingekuwa na ndege, ninawaomba ATCL mumsafirishe bure mzee Mapunda kwa kazi kubwa aliyoifanya ." amesema Rais Ma...

NDEGE YA TANZANIA AIR-BUS A220 YATUA ACCRA, KUTUA KESHO DAR ES SALAAM

Ndege ya kwanza kati ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania imewasili Mjini Accra nchini Ghana ikiwa safarini kuja hapa nchini. Ndege hiyo itawasili kesho majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.   Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Mhe. Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo imetua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege. Balozi Mboweto wafanyakazi na baadhi ya abiria waliokuwapo katika uwanja huo wameonesha shauku kubwa ya kutaka kuiona ndege hiyo ambayo ni ya kwanza kutua Barani Afrika tangu kampuni ya Air-Bus ianze kutengeneza ndege za kizazi cha A220.   “Wafanyakazi wa hapa uwanja wa ndege na baadhi ya abiria baada ya kutangaziwa kuwasili kwa ndege hii aina ya A220 wamekuwa na shauku kubwa ya kuiona na kwa kweli ni ndege nzuri inapendeza na inawavutia zaidi kumuona T...

Tanzania yatia saini ujenzi wa mradi wa umeme unaopigiwa kelele na wanamazingira, Rais Magufuli asema ni mradi wa lazima kwa maendeleo

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa Stigler's Gorge ni jambo la lazima. Leo rais wa nchi hiyo John Magufuli ameweka saini na wakandarasi wa mradi huo kutoka Misri wakiwa pamoja na waziri mkuu wa nchi yao. Hatua hiyo inakuja baada ya miaka 40 tangu utafiti wa uzalishaji wa umeme kutoka mto Rufiji ambao unaweza kuzalisha megawati 2,100 kufanyika wakati huo Tanzania ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere. Mradi huu unatarajiwa kutekelezwa na fedha za watanzania wenyewe kwa kiwango cha dola za kimarekani bilioni 2.9 ambayo ni sawa na takribani shilingi trilion 6.5 za kitanzania. Na kampuni itakayofanya kazi hiyo inatoka Misri. Rais Magufuli amesema kwamba walitumia muda kutafakari kuhusu mradi huu kwa sababu Tanzania imebarikiwa na vyanzo vingi sana vya uzalishaji umeme kama vile maji,gesi asilia,upepo,joto ardhi ,makaa ya mawe pamoja na madini ya urani. Na kufikia uamuzi huo wal...