Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje wa Uingereza akosoa Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania Waziri Kivuli wa Mambo ya nje wa Uingereza Liz McInnes aimeikosoa Sheria ya Vyama vya Siasa Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje wa Uingereza ameeleza kusikitishwa kwake na kupitishwa kwa sheria ya vyama vya siasa nchini Tanzania ambayo anadai inaminya vyama vya upinzani. Liz McInnes ambaye ni mbunge kupitia chama cha upinzani Labour amekaririwa na mtandao wa chama chake akisema wapinzani inabidi waachiwe uhuru wao . ''Inasikitisha kusikia kuwa bunge la Tanzania limepitisha sheria ambayo inazuia vikali shughuli za kisiasa na kutoa mamlaka kwa msajili wa vyama vya siasa kuvifutia usajili vyama vya upinzani''. ''Wanasiasa wa upinzani wanapaswa kuwa na uhuru wa kuipa changamoto serikali na si kuhofia kufungwa kwa kutoa maoni yao ikizingatiwa kuwa kuna chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzji mkuu mwakani''. Mwanasiasa huyo ametahadharisha kuwa mat...