Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kuongoza kikao cha halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi kitakachofanyika Jijini Dar es salaam ambacho kitalenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya kisiasa nchini. Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kikiongozwa na Mwenyekiti wake Rais John Magufuli. Jana jioni Desemba 17, Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi aliongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho ambacho kilifanyika Jijini Dar es salaam, ambapo kabla ya kikao hicho, kilitanguliwa na kikao cha kamati ya usalama ya maadili. Hivi karibuni kuliibuka mvutano wa maneno baina ya Katibu Mkuu wa CCM na Dkt Bashiru Ally na moja ya Kada mkongwe wa chama hicho Bernard Membe ambaye alitajwa kupanga njama za kumuhujumu Mwenyekiti wake Rais Magufuli hali ambayo ilimfanya Dkt Bashiru kumuita kada huyo. Membe ni mmoja ya wanaotajwa kuwa huenda akawa ni miongoni mwa watakaojadiliwa kwenye vikao hivyo kutokana na mwenendo wake wa kisias...