Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wabunge 19 Chadema kulinda kura Dodoma

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamesema watawatumia wabunge kumi na tisa wa chama hicho kulinda kura katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kizota katika jiji la Dodoma. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma ā€¦ (endelea).


Viongozi walitoa kauli hiyo jana nje ya ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kizota muda mfupi baada ya mgombea udiwani kata hiyo kupitia Chadema, Omar Bangababo kurejesha fomu ya ugombea kata hiyo.


Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Chadema Kanda ya Kati, Iddy Kizota amesema watawatumia wabunge wa Chadema kulinda kura za mgombea kutokana na kuwapo kwa hujuma za kuwapiga mawakala na kuwaondoa vituoni kwa lengo la kubadilisha matokeo.

Hata hivyo Kizota amesema kulikuwepo na njama kubwa ambazo zilikuwa zikifanywa na Ofisi Mtendaji wa Kata ya Kizota, Loyce Mrefu kwa kutaka kumkwamisha mgombea wa Chadema kwa kumwekea vikwazo visivyokuwa na sababu.

ā€œUnaweza kujiuliza msimamizi wa uchaguzi anakuwa na visingizio kibao kwa kudai kuwa ofisi ya kata haina daftari ya orodha ya wapiga kura, mara hakuna risiti kwa kwa ajili ya kumpatia mgombea pamoja na mambo kadha wa kadha,ā€ amesema Mrefu.

Amesema kutokana na kuwapo dalili za hujuma ambazo zinafanywa na viongozi wa chama tawala kwa kushirikiana na watumishi wa serikali wamejipanga kuhakikisha wanalinda na kusimamia sheria, kanuni na misingi yote ya uchaguzi.

Hata hivyo Afisa Mtendaji wa Kata ya Kizota, Loyce Mrefu alipoulizwa juu malalamiko ya wanayoelezwa na wanachama wa Chadema alisema yeye siyo msemaji wa uchaguzi ingawa ni Ofasa Mtendaji kata.

Pamoja na kudai kuwa siyo msemaji alieleza kuwa vyama vilivyochukua fomu na kurejesha mpaka ni vyama siasa ni CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF, UDPD na NLD.

Kwa upande wa mgombea udiwani kata ya Kizota kupitia Chadema, Omar Bangababo amesema amenitosa kuwania nafasi hiyo ili kupambana na changamoto ambazo mtangulizi wake ameshindwa kuzitatua kutokana na kukosa msimamo kwa wananchi walio mchagua

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...