Wine alifikishwa katika mahakama ya jeshi mjini Gulu ambapo maamuzi hayo yalitolewa baada ya serikali kumshtaki kwa kumiliki bunduki kinyume cha sheria
- Kuachiliwa huru kwake kwa muda kuliwadia baada ya shinikizo tele kutoka kwa raia na hali tete kuendelea kushuhudiwa nchini Uganda
- Wine alikamatwa tena mara baada ya kuachiliwa huru na kuwasilishwa katika mahakama ya raia na sasa ataendelea kuiziliwa hadi Agosti 30, 2028
Serikali nchini Uganda imeondoa mashtaka ya uhaini dhidi ya Mbunge wa Kyadondo Mashariki Robert Kyagulanyi, almaarufu Bobi Wine, kufuatia hali tete na ghasia zilizoshuhudiwa nchini humo kutoka kwa raia waliotaka aachiliwe huru.
Wine, ambaye amekuwa kizuizini kwa muda wa wiki moja sasa, alipewa uhuru huo wa muda katika mahakama ya jeshi mjini Gulu, Alhamisi, Agosti 23, na kukamatwa tena.
Maandamano yamekuwa yakishuhudiwa maeneo mbalimbali nchini Uganda na pia Kenya yakilenga kuishinikiza serikali ya Uganda kumwachilia huru Bobi Wine. Picha: NTV Uganda.
TUKO.co.ke imethibitisha mwanasiasa huyo mwasi dhidi ya serikali ya Raia Yoweri Museveni, alikamatwa mara baada ya kuachiliwa huru na kuwasilishwa katika mahakama ya raia, licha ya wafuasi na wakili wake kulalamika.
āHamna sababu yoyote ya kusema Kyagulanyi anatafutwa na polisi ama kuna mashtaka yoyote dhidi yake. Naomba usiifanye korti hii kuwa korti ya kukamata na kumpa Mhe Kyagulanyi uhuru wake,ā wakili wa Wine, Medard Ssegona alisema.
Hali ya maandamano na ghasia imeshuhudiwa nchini Uganda tangu kakamatwa kwake wiki moja iliyopita na kumekuwapo na madai kuwa, Wine aliteswa akiwa korokoroni.
Mwanasiasa huyo anayempa wakati mgumu Museveni, alikamatwa kwa madai ya kuhusika na ghasia zilizosababisha msafara wa rais kupigwa mawe mjini Arua, Kaskazini mwa Uganda.
Museveni alikuwa Arua akimpigia debe mwaniaji wa chama chake Nusura Tiperu, wakati Bobi Wine alipokuwa akimpigia kampeini mwaniaji Huru, Kassiano Wadri, na ghasia zikazuka. Polisi walifyatua risasi na kumuua dereva wa Wine na watu wengine watano.
Maoni