Rais wa Tanzania afiwa na dada yake


Rais Magufuli alipoenda kumtembelea dada yake akiwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU)

Dada yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia leo tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza.


Hapo jana Rais Magufuli alienda kumtembelea dada yake akiwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) katika hospital hiyo ya Bugando na rais alisema kwamba hali ya dada yake sio nzuri.


Bi.Monica Magufuli alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo.


Monica Joseph Magufuli amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63 (alizaliwa tarehe 25 Novemba, 1955) na ameacha watoto 9 na wajukuu 25


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU