Mgombea wa Upinzani ajitangaza Mshindi Mgombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu wa Cameroon Maurice Kamto anadai kuwa ameshinda uchaguzi wa uraisi wa siku ya jumapili licha ya onyo la serikali dhidi ya hatua hiyo. Kamto ambaye ni kiongozi wa chama cha Rebirth of Cameroon (MRC), ametoa wito kwa rais Paul Biya kuachia madaraka kwa amani. Akizungumza na waandishi wa habari mji mkuu wa Yaounde amesema ''Namuomba rais anayeondoka kupanga namna ya kumpokeza madaraka mpizani wake kwa amani.'' Mgombea huyo wa upinzani hakutoa matokeo ya kuthibitisha madai yake japo wafuasi wake walimshangilia kwa vifijo wakati alipokua akitoa tangazo hilo. Uchaguzi huo umeonekana na wenga kama mpango wa kurefusha utawala wa rais Biya ambaye ni mmoja wa viongozi wa Afrika waliyoshikilia madaraka kwa muda mrefu. Naibu katibu mkuu wa wa chama tawala cha Cameroon People's Democratic Movement, Gregoire Owona, amemshutumu Kamto kwa uvunjaji sheria. "Kamto hakuweka ...