Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 12, 2017

Raia wajitokeza kumshinikiza Mugabe kujiuzulu Zimbabwe

Maelfu ya raia wa Zimbabwe wamejitokeza barabarni hasa mjini Harare wakijiandaa kwa mkutano mkubwa unaoungwa mkono na chama tawala ZANU-PF katika jitihada za kuongeza shinikizo za kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu,wakishikilia mabango yaliyoandikwa Mugabe Must Go. Zanu-PF ndio chama kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40. Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko mkubwa katika chama tawala. Kikubwa kinachozozaniwa ni nani atakayemrithi rais Mugabe atakapoochia madaraka. Jeshi la nchi hiyo lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina. MUgabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa madaraka. Zaidi ya hayo Bw. Mugabe angependa kuendelea kuwa u...

Pentagon yamtaka Trump kujiuzulu kimakosa Ndio idara inayosimamia nambari za siri makombora, Idara inayosimamia usalama wa Marekani na mkuu wake ni rais wa Marekani ambaye hupendelea sana kutumia mtandao wa Twitter

Pentagon yamtaka Trump kujiuzulu kimakosa Ndio idara inayosimamia nambari za siri makombora, Idara inayosimamia usalama wa Marekani na mkuu wake ni rais wa Marekani ambaye hupendelea sana kutumia mtandao wa Twitter Ujumbe huo ambao pia uliwataka wanasiasa wengine wawili wa Marekani kujiuzulu kufuatia madai ya unyanyasaji wa kijinsia ulitumwa kutoka kwa akaunti ya @ProudResister Ndio idara inayosimamia nambari za siri makombora, Idara inayosimamia usalama wa Marekani na mkuu wake ni rais wa Marekani ambaye hupendelea sana kutumia mtandao wa Twitter. Lakini inapofikia wakati wa kusimamia akaunti yake ya mtandao huo, the Pentagon inafaa kuimarisha uwezo wake. Siku ya Alhamisi idara hiyo ya ulinzi ilituma ujumbe kimakosa katika mtandao wake wa Twitter ukimtaka rais Trump kujiuzulu. Ujumbe huo ambao pia uliwataka wanasiasa wengine wawili wa Marekani kujiuzulu kufuatia madai ya unyanyasaji wa kijinsia ulitumwa kutoka kwa akaunti ya @ProudResister, mwanaharakti ambaye ni mkosaji mkuu wa...

Pogba na Ibrahimovic kucheza dhidi ya Newcastle Jumamosi

Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wataorodheshwa katika kikosi cha Manchester United katika mechi ya Jumamosi ya ligi ya Uingereza dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Old Trafford Zlatan Ibrahimovic na Zlatan Ibrahimovic Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wataorodheshwa katika kikosi cha Manchester United katika mechi ya Jumamosi ya ligi ya Uingereza dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Old Trafford. Mshambuliaji Ibrahimovic , 36, bado hajashirikishwa katika mechi yoyote msimu huu baada ya kupata jeraha la goti mnamo mwezi Aprili. Kiungo wa kati Paul Pogba , 24, hajaichezea timu yake tangu alipopata jeraha la nyuma ya goti dhidi ya klabu ya Basel mnamo mwezi Septemba. Beki Marcos Rojo pia anapatikana na mkufunzi Jose Mourinho alisema kuwa wote wataorodheshwa. ''Paul unaweza kuona. Unaweza kugundua kwamba kulikuwa na Manchester United msimu huu kabla na hata baada ya jeraha lake'', aliongezea Mourinho. ''Ana uwezo ambao hubadilisha vile tutakavyocheza mechi z...

HECHE AMSHUKURU SPIKA KWA KUMLINDA ASIKAMATWE

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amekiri bila busara za Spika wa Bunge kutumika leo angekuwa amekamatwa leo na polisi wamedaiwa kutoka Morogoro waliokuwa eneo la Bunge kwa nia ya kumkamata. Mh. Heche amweka hilo wazi jioni hii huku akikosoa matumizi mabaya ya rasilimali iliyotumiwa. "Nimepokea barua ya polisi asubuhi leo wakinitaka kuripoti Morogoro eti kwa kosa la kumsindikiza na kufanya mkutano jimboni kwa Mh Lijualikali alipotoka gerezani mwezi wa 4" Amesema Heche na kuongeza; "Kabla hata ya kuitikia wanataka kunikamata bila busara za spika wangenikata. Matumizi mabovu ya rasilimali" Kabla ya taarifa hii kutoka Mapema leo Heche alikiri kupokea wito unaomtaka kwenda kuhojiwa Morogoro. "Nimepewa wito kuwa natakiwa nikahojiwe Morogoro. Nimepokea wito huu na tayari nao wako hapa. Siamini kama Spika ataruhusu hili," amesema Heche.

Mugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza

Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi Mugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano. Alihudhuria sherehe za kufuzu kwenye mji mkuu Harare. Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi. Jeshi lilisema Ijumaa kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazunngumoz hayo haraka iwezekanavyo. Mtu moja aliyeshuhudia alinukuliwa na Reuters akisema kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza. Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kmfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua ungonizi wa Zanu-PF na urais.

HISTORIA YA MAISHA YANGU NILIPOKUWA URUSI KAMA NILIVYOSIMULIA NIKIWA GLOBAL PUBLISHERS,SEHEMU YA 1

MJUE DR. LOUIS SHIKA HISTORIA YA MAISHA YANGU NILIPOKUWA URUSI KAMA NILIVYOSIMULIA NIKIWA GLOBAL PUBLISHERS,SEHEMU YA 1 Dkt. Louis Shika ambaye amepata umaarufu mkubwa baada ya kushiriki katika mnada wa nyumba za Said Lugumi jijini Dar es Salaam na baadaye ‘kukwaruzana’ na jeshi la polisi kutokana na mchakato wa mnada huo, amefunguka engi kuhusu maisha yake. Katika simulizi hiyo, Dkt Shika ambaye hivi sasa ni maarufu kama ‘900 Itapendeza’ kutokana na mambo yaliyojiri katika mnada huo, alianza kwa kusema kwamba neno ‘daktari’ linalotangulia jina lake ni la kitaalam, yaani kweli yeye ni daktari wa binadamu akiwa alisomea taaluma hiyo nchini Urusi. “Nilisomea utaalam huo nchini Urusi nilikokwenda mwaka 1984 kwenda kuchukua digrii ya kwanza ya miaka saba ambayo niliimaliza mwaka 1991,” anasema daktari huyo mwenye mwili wa kiasi na kimo kirefu. Anaendelea kusema kwamba mwaka huohuo aliamua kuunganisha masomo apate digrii ya pili ya mag...

Mamba' ambaye amegeuka kumuuma Mugabe

Mnangagwa alisaidia kuongoza vita vya kupigania uhuru vya Zimbabwe na baadaye kuwa jasusi mkuu wa nchi wakati wa mgogoro wa ndani kwa ndani ambapo maelfu wa wananchi waliuwawa.   Mnangagwa amekuwa miongoni mwa waliotarajiwa kumrithi Mugabe Imekuwa siri ya wazi nchini Zimbabwe kwa miaka mingi kuwa Emmerson Mnangagwa angechukua nafasi ya Robert Mugabe na kuwa rais. Lakini Bwana Mugabe alionekana kucheza na hisia zake- wakati mwingine akimpandisha cheo ndani ya chama tawala cha Zanu- PF na serikalini na kuongeza tetesi ya yeye kuwa mrithi mtarajiwa lakini baadaye alishushwa cheo baada ya Mnangagwa kuonekana kuonesha nia zake mapema mno. Baada ya kutenguliwa, imeonekana kama subira ya mwanaume huyo maarufu kama "mamba" hatimaye imeisha. Baada ya Rais Mugabe kumtengua na kumshutumu kwa mfisadi, wafuasi wake na vikosi vya usalama waliingilia kati kwa niaba yake. Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe Constantino Chiwenga (kushoto) ni rafiki wa karibu wa Mnangagwa Mnangagwa ...

Picha Kutoka Eneo la Ajali ya Ndege iliyoua watu 11 Ngorongoro Arusha

Jeshi la Polisi Arusha limepata miili ya watu 11 waliofariki kwenye ajali ya ndege ndogo ya Coastal Aviation iliyotokea November 15, 2017 katika eneo la Embakazi Wilayani Ngorongoro. Ndege hiyo ilipaa kutoka uwanja mdogo wa Arusha saa nne na dakika 10 asubuhi kuelekea uwanja wa Ndege Kilimanjaro (KIA) na kuchukua abiria watano jumla ikawa na abiria 10 na Rubani akiwa ni mtu wa 11 kwenye ndege hiyo na kuelekea Ngorongoro.

Mugabe 'akataa wito wa kumtaka ajiuzulu'

Mugabe, 93 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani wakati jieshi lilichukua madaraka siku ya Jumatano kufuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi. Mugabe (wa pili kulia) akiwa kuzuizi cha nyumbani akisimama na mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga (kulia) Rais wa miaka mingi nchini Zimbabwe anaripotiwa kukataa kuandoka madarakana mara moja licha ya kuongezeka wito wa kumtaka ajiuzulu. Mugabe, 93 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani wakati jieshi lilichukua madaraka siku ya Jumatano kufuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi. Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo yaliyofanywa Muganbe na ujumbe kutoka kanda hiyo pamoja na mapema. Lakini taarifa zinasema kuwa amekataa kuondoka madarakani. Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai alisema mapema kuwa kwa manufaa ya watu Mugabe anastahili kujiuzulu mara moja. Robert Mugabe alikutana na mkuu wa majeshi aliyeongoza hatua dhidi yake Jeshi lilichukua hatua baada ya Rais Mugabe kumfuta makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa, wiki ili...

Kampuni ya Uswisi yafungua kiwanda cha kemikali Tanzania

Kampuni kutoka nchini Switzerland imefungua kiwanda cha kemikali za ujenzi na zile zinazotumika katika magari.   Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli Kampuni kutoka nchini Uswisi imefungua kiwanda cha kemikali za ujenzi na zile zinazotumika katika magari. Florence Tinguely Mattli ni balozi wa Uswisi nchini Tanzania, ameiambia BBC kuwa suala la uwekezaji ni hatua ya kujiamini kwanza na kutoona hasara. Alipoulizwa kuhusiana na sera za uwekezaji nchini Tanzania kudaiwa kuwa si rafiki Bi.Mattli amesisitiza kuwa uzoefu wao kiviwanda na kuwekeza katika mataifa mbalimbali duniani itawasaidia kujua ni mambo gani ya kuzingatiwa katika uwekezaji wao Tanzania katika serikali ya awamu ya sasa. Kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya elfu moja Waziri wa viwanda wa Tanzania Dr Charles Mwijage anasema kuwa dira ya mwaka 2025 ni kuhusiana na viwanja. Meneja mkuu wa kiwanda hiki cha Kemikali cha Sika Tanzania Alfonso Paradinas anasema kiwanda ch...

Miito yaongezeka kumtaka Mugabe kuachia ngazi, Zimbabwe

Raia nchini Zimbabwe wameanza kuangazia mustakabali wa taifa hilo bila ya kiongozi wao aliyekaa madarakani kwa takriban miongo minne, wakati mazungumzo ya maridhiano yakiendelea. Raia nchini Zimbabwe wameanza kuangazia mustakabali wa taifa hilo bila ya kiongozi wao aliyekaa madarakani kwa takriban miongo minne. Jeshi limechukua nafasi ya rais Robert Mugabe mwenye miaka 93, shujaa wa ukombozi aliyegeuka kuwa mtawala wa kiimla, ambaye kwa sasa yuko katika kizuizi cha nyumbani. zaidi kuhusu kinachojiri Zimbabwe. Taifa hilo liliachwa na mshangao baada ya rais huyo mkongwe kuwekwa katika kizuizi cha nyumbani jioni ya Jumanne, na wanajeshi kuweka doria kwenye maeneo muhimu katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, na maafisa wake waandamizi kutangaza kuchukua udhibiti wa kituo cha televisheni. Kiongozi wa upinzani aliyerejea nchini humo, Morgan Tsvangira amesema ni lazima rais Robert Mugabe ajiuzulu. Ametaka serikali ya mpito kujadiliwa, na kuhusisha pande zote pamoja na kufanywa mageuzi mapa...

Pogba muhimu zaidi United: Majeraha yake yalivyowagharimu Lukaku & Mhikitaryan

Baada ya mwanzo mzuri katika msimu huu akifunga magoli 11 katika mechi 10 za kwanza, Romelu Lukaku alitegemewa kuendeleza moto wa ufungaji, hata hivyo tangu alipofunga goli lake la 7 katika Premier League mnamo September 30, Lukaku amepatwa na ukame mkubwa, akicheza mechi 7 mfululizo katika mashindano yote bila kufunga goli. Wakati suala la ukame ni jambo la kawaida ambalo linawakuta washambuliaji wengi – Robin Van Persoe alicheza mechi 13 chini ya Sir Alex Ferguson bila kufunga – jambo linalompa wakati mgumu Jose Mourinho kuhusu hali ya uchezaji kiujumla ya Lukaku, hasa tangu Paul Pogba alipopata majeruhi. Katika mchezo wa mwisho wa Manchester United katika EPL, dhidi ya Chelsea, Lukaku aligusa mpira mara 24 tu. Alishindwa kujihusisha zaidi na mchezo na alikuwa amepotezwa kabisa. Sio ya makosa yake yote, sapoti kutoka kwa viungo wake haikuwa inayojitosheleza, kwa kifupi haukuwa mchezo mzuri kwake. Ukiangalia upande wa Bluu Alvaro Morata, aligusa mpira mara 51, hapa utao...

FIFA waikataa rekodi ya Romelu Lukaku na kupunguza mabao yake.*

Mashabiki wa Ubelgiji na Manchester United jana walijawa na furaha baada ya kusikia kwamba mshambuliaji wao Romelu Lukaku amevunja rekodi ya ufungaji katika timu yao ya taifa. Romelu Lukaku alitajwa kuvunja rekodi hiyo kwa kuwapita Bernard Voorhoof na Paul Van Himst ambao wana mabao 30 huku goli dhidi ya Japan likimfanya yeye kufikisha 31 idadi ambayo hata Lukaku mwenyewe alijinasibu kuifikia. Lakini sasa shirikisho la soka duniani FIFA limeibuka na kutoitambua rekodi hiyo ya Romelu Lukaku kwa kusema kwamba moja kati ya michezo ambayo Lukaku alifunga hautambuliki na shirikisho hilo. Mechi hiyo ilikuwa mwaka 2014 ambapo Ubelgiji walicheza dhidi ya timu ya taifa ya Luxembourg ambapo Ubelgiji waliibuka kidedea kwa mabao 5 huku Romelu Lukaku akifunga mabao 3 kati ya hayo 5. Kinachowafanya FIFA kuundoa mchezo huo kwenye rekodi zao ni kitendo cha Ubelgiji kufanya sub 7 badala ya 6 katika mchezo huo suala ambalo lilikuwa kinyume na sheria katika mechi hiyo. Hii sasa inamaanisha Lukaku a...

FULL HIGHLIGHTS- BENIN 1-1 TANZANIA (12-11-2017

MTEULE THE BEST

Mwigizaji wa Tanzania Lulu Elizabeth miaka miwili ya kifungo cha kuua nyota wa bongo Steven Kanumba

Elizabeth Lulu na Steven Kanumba Tanzania: Lulu alipigwa kwa muda wa miaka miwili ya jela la kuua Kanumba Dar es Salaam - Mahakama Kuu imemhukumu Elizabeth Elizabeth aliwahi Lulu kwa muda wa miaka miwili ya jela baada ya kupata hatia ya kusababisha kifo cha muigizaji Stephen Kanumba. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Sam Rumanyika Jumatatu, Novemba 13 asubuhi. Mahakama ilimuona kuwa na hatia ya kutenda kosa, ambalo linapingana na kifungu cha 195 cha Kanuni ya Adhabu. Bw Kanumba, ambaye alikuwa mmoja wa wahusika wengi wa ndani, alikufa Mwigizaji wa Tanzania Lulu Elizabeth ametolewa kwa miaka miwili ya jela kwa ajili ya mauaji Lulu alihukumiwa na mahakama ya Dar es Salaam kwa kuua muigizaji Steven Kanumba Kanumba alikufa mwaka 2012 baada ya kushindana na Lulu Migizaji wa Tanzania amefungwa kwa muda wa miaka miwili ya jela baada ya kupatikana na hatia ya kuua mwigizaji mwenzake Steven Kanumba mwaka 2012. Mahakama Kuu ya Dar es Salaam iligundua Elizabeth Lulu Michaels mwenye hatia ya...

Waziri mkuu Uhispania aapa kumaliza mzozo wa Catalonia

Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Waziri mkuu Mariano Rajoy (kushoto) Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amesema kuwa uchaguzi wa eneo la Catalonia mwezi ujao utasaidia kumaliza mzozo wa kijitenga katika eneo hilo la kaskazini mashariki mwa nchi. Alihutubia mkutano wakati wa ziara yake ya kwanza tangu kutangaza udhibiti kamili eneo hilo. Viongozi kadhaa waku wa Catalonia kwa sasa wanazuiliwa kufuatia hatua hiyo. Aliyekuwa kiongozi wa Catalonia ajisalimisha kwa polisi Takriban watu 75,000 waliandamana mjini Barcelona siku ya Jumamosi kupinga kukamatwa viongozi hao. Hali hiyo ilichochewa na kura ya maoni iliyokumbw na utata ilyofanyika Catalonia mwezi Oktoba ambayo ilikuwa imezuiwa na mahakama za Uhispania. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Takriban watu 75,000 waliandamana mjini Barcelona siku ya Jumamosi kupinga kukamatwa viongozi hao. Maafisa huko Catalonia walisema kuwa kura hiyo ilipata asilimia 92 ya ...

Vita vya maneno vyazuka tena kati ya Trump na Korea Kaskazini

Rais wa Marekani na Korea Kaskazini wamerejelea vita vyao vya maneno kufuatia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini. Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni wa Korea Kaskazini ilimuita Trump kuwa "mchochezi wa vita na mzee" na kusisitiza kuwa haiwezi kamwe kuachana na mipango yake ya nyuklia. Rais Trump alijibu kwa kuandika katika mtandao wake wa kijamii wa Tweeter kuwa, anashangaa ni kwa namna gani Kiongozi wa Korea Kaskazini anamuita mzee. Trump: Ni kitu kimoja tu kitafanya kazi dhidi ya Korea Kaskazini CIA: Hakuna uwezekano wa kutokea vita vya nuklia na Korea Kaskazini Korea Kaskazini: CIA wanapanga kumuua Kim Jong-un Kile unachohitaji kufahamu kuhusu Korea Kaskazini Kwa maneno yake, Bwana Trump alisema kuwa hatamuita Rais Kim Jong-un, kuwa mtu "mfupi na mnene". Anasema kuwa anajaribu sana kwamba siku moja atakuwa rafiki wake wa karibu. Trump awali alimkejeli kiongozi huyo mkuu wa Korea Kaskazini, kwa kumuita mwendawazimu na 'mtu wa kuunda zana za roket...

Lukaku afikia rekodi hii Ubelgiji

Mshambuliaji wa Manchester United Romelo Lukaku amesema amezaliwa kufunga na anaamini ataendelea kufanya hivyo pamoja na kuvunja rekodi ufungaji bora nchini Ubelgiji kabla ya mwaka huu kuisha. Lukaku ameyasema hayo baada ya kuifikia rekodi ya Paul Van Himst na Bernard Voorhoof ya mabao 30 katika timu ya taifa ya Ubelgiji, ambapo ameeleza kuwa bado ana nia ya kufunga zaidi. “Nimezaliwa kwa ajili ya hili na nitaendelea kufanya hivyo", amesema Lukaku ambaye sasa anahitaji bao moja tu kuweza kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wa nchini ya Ubelgiji. Lukaku alifunga mabao mawili kwenye sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mexico hivyo kufikisha mabao 30 sawa na Paul Van Himst na Bernard Voorhoof ambao wanashikilia rekodi hiyo. Lukaku anafanya vizuri msimu huu akiwa na Manchester United ambapo tayari amefunga mabao saba kwenye ligi kuu soka nchini England. Lukaku anaweza kuvunja rekodi siku ya jumanne ambapo Ubelgiji itacheza mechi ya kirafiki na Japan.

Mchezaji wa bora wa Afrika taji la BBC mwaka 2017: Mpigie kura unayempenda

 Upigaji kura wa mchezaji atakayeshinda taji la mchezaji bora wa Afrika la BBC mwaka 2017 umeanza. Wachezaji watano walioorodheshwa ni Pierre-Emerick Aubameyang, Naby Keita, Sadio Mane, Victor Moses naMohamed Salah. Walitangazwa katika kipindi maalum cha moja kwa moja katika BBC. Waliowahi kushinda tuzo hiyo awali ni pamoja na nyota wawili wa Ivory Coast Didier Drogba na Yaya Toure, Jay-Jay Okocha wa Nigeria na jagina wa Liberia George Weah. Jopo ambalo liliwashirikisha miongoni mwa wengine Emmanuel Amuneke, mshindi wa ubingwa Afrika na Olimpiki 1996, Arnaud Djoum, mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 akiwa na Cameroon, na Jean Sseninde, kutoka Uganda anayechezea Crystal Palace Ladies, walikuwepo kujadili majina ya walioteuliwa kushindania tuzo hiyo. Watano hao watakuwa wakitumai kufuata nyayo za mshindi wa mwaka jana Riyad Mahrez, aliyeng'aa mwaka 2016 akichezea mabingwa wa Ligi ya Premia mwaka huo Leicester City na Algeria. Mashabiki wanaweza kupigia mchezaji wana...