Haki miliki ya picha
REUTERS
Image caption
Waziri mkuu Mariano Rajoy (kushoto)
Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amesema kuwa uchaguzi wa eneo la Catalonia mwezi ujao utasaidia kumaliza mzozo wa kijitenga katika eneo hilo la kaskazini mashariki mwa nchi.
Alihutubia mkutano wakati wa ziara yake ya kwanza tangu kutangaza udhibiti kamili eneo hilo.
Viongozi kadhaa waku wa Catalonia kwa sasa wanazuiliwa kufuatia hatua hiyo.
Aliyekuwa kiongozi wa Catalonia ajisalimisha kwa polisi
Takriban watu 75,000 waliandamana mjini Barcelona siku ya Jumamosi kupinga kukamatwa viongozi hao.
Hali hiyo ilichochewa na kura ya maoni iliyokumbw na utata ilyofanyika Catalonia mwezi Oktoba ambayo ilikuwa imezuiwa na mahakama za Uhispania.
Haki miliki ya picha
REUTERS
Image caption
Takriban watu 75,000 waliandamana mjini Barcelona siku ya Jumamosi kupinga kukamatwa viongozi hao.
Maafisa huko Catalonia walisema kuwa kura hiyo ilipata asilimia 92 ya kura kutoka kwa watu asilimia 43 waliojitokeza.
Wengi wa wale waliopinga kura hiyo hawakupiga kura na walikataa kutambua uhalali ya kura hiyo.
Hali ya kisiasa si shwari Catalonia
Serikali ya Catalonia hatimaye ikatangaza uhuru. Kujibu hilo serikali ya Uhispania ilivunja bunge la Catalonia na katangaza udhibiti kamili na kuitisha uchaguzi wa mapema tarehe 21 Disemba
Maoni