Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kampuni ya Uswisi yafungua kiwanda cha kemikali Tanzania





Kampuni kutoka nchini Switzerland imefungua kiwanda cha kemikali za ujenzi na zile zinazotumika katika magari.





 







Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli



Kampuni kutoka nchini Uswisi imefungua kiwanda cha kemikali za ujenzi na zile zinazotumika katika magari.

Florence Tinguely Mattli ni balozi wa Uswisi nchini Tanzania, ameiambia BBC kuwa suala la uwekezaji ni hatua ya kujiamini kwanza na kutoona hasara.

Alipoulizwa kuhusiana na sera za uwekezaji nchini Tanzania kudaiwa kuwa si rafiki Bi.Mattli amesisitiza kuwa uzoefu wao kiviwanda na kuwekeza katika mataifa mbalimbali duniani itawasaidia kujua ni mambo gani ya kuzingatiwa katika uwekezaji wao Tanzania katika serikali ya awamu ya sasa.



Kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya elfu moja

Waziri wa viwanda wa Tanzania Dr Charles Mwijage anasema kuwa dira ya mwaka 2025 ni kuhusiana na viwanja.

Meneja mkuu wa kiwanda hiki cha Kemikali cha Sika Tanzania Alfonso Paradinas anasema kiwanda chake kitazalisha kemikali hizo za ujenzi na kuongeza ubora wa majengo nchini humo.

Hata hivyo kwa upande wake Meneja wa kanda ya Sika ya Ulaya, Mashariki ya kati na Afrika Ivo Schaedler lengo lao ni kutumia soko la Tanzania na kuongeza ufanisi nchini humo,na kuongeza kuwa wana viwanda 17 ndani ya Afrika


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...