Mnangagwa alisaidia kuongoza vita vya kupigania uhuru vya Zimbabwe na baadaye kuwa jasusi mkuu wa nchi wakati wa mgogoro wa ndani kwa ndani ambapo maelfu wa wananchi waliuwawa.
Mnangagwa amekuwa miongoni mwa waliotarajiwa kumrithi Mugabe
Imekuwa siri ya wazi nchini Zimbabwe kwa miaka mingi kuwa Emmerson Mnangagwa angechukua nafasi ya Robert Mugabe na kuwa rais.
Lakini Bwana Mugabe alionekana kucheza na hisia zake- wakati mwingine akimpandisha cheo ndani ya chama tawala cha Zanu- PF na serikalini na kuongeza tetesi ya yeye kuwa mrithi mtarajiwa lakini baadaye alishushwa cheo baada ya Mnangagwa kuonekana kuonesha nia zake mapema mno.
Baada ya kutenguliwa, imeonekana kama subira ya mwanaume huyo maarufu kama "mamba" hatimaye imeisha. Baada ya Rais Mugabe kumtengua na kumshutumu kwa mfisadi, wafuasi wake na vikosi vya usalama waliingilia kati kwa niaba yake.
Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe Constantino Chiwenga (kushoto) ni rafiki wa karibu wa Mnangagwa
Mnangagwa alisaidia kuongoza vita vya kupigania uhuru vya Zimbabwe na baadaye kuwa jasusi mkuu wa nchi wakati wa mgogoro wa ndani kwa ndani ambapo maelfu wa wananchi waliuwawa.
Amekanusha kuhusika wowote katika mauaji hayo na kuilaumu jeshi.
Hata hivyo, hamna matumaini kuwa vitendo vya kukiuka wa haki za binadamu vitasitishwa chini ya utawala wake. Wakosoaji wake wanasema Mnangagwa ana damu mikononi mwake.
Anajulikana kama "mamba" sababu ya kizimu cha jamii yake; jina ambalo linaokenana kumfaa.Kwa maana hiyo, wafuasi wake hufahamika kama "Lacoste"
Emmerson Mnangagwa ni nani ?
•Anajulikana kama "mamba" sababu ya kizimu cha jamii yake. , wafuasi wake wanafahamika kama "Lacoste"
•Alipata mafunzo ya jeshi nchini China na Misri
•Aliteswa na vikosi vya Rhodesia baada ya mashambilizi yake ya kiaina
•Alisaidia kuongoza kupigania uhuru nchi ya Zimbabwe miaka ya 70
•Alikuwa mjasisi wa nchi wakati wa mgogoro wa ndani kwa ndani ambapo maelfu wa wananchi waliuwawa.
•Anaojulikana lama muunganishi baina ya jeshi, idara ya ujasisi na chama cha Zanu- PF
•Anatuhumiwa kwa kuwa nyuma ya mashambilio dhidi ya wafuasi wa upinzania baada ya uchaguzi wa 2008
Walipigania uhuru Zimbabwe miaka ya 1970 wametawala siasa za nchi hiyo
Wale waliopigana katika vita ya miaka 70, kama Bw. Mnangagwa, wamehodhi madaraka kwa muda mrefu nchini Zimbabwe,huku wakiogopa kupoteza vyeo vyao kama Grace Mugabe angemritihi mume wake,kwa hio waliingilia kati.
Wakati rafiki wake wa karibu , Jenerali Constantino Chiwenga alionya dhidi ya 'vitendo vya vinavyolenga kuwatoa wanachama waliopiginia uhuru wa taifa' ilikuwa wazi kwamba alikuwa akizungumzia kufukuzwa kazi kwa Mngangagwa.
Uhusiano na Congo
Bw Mnangagwa alizaliwa mkoa wa kati wa Zvishavane na anatokea jamii ya Karanga iliyo jamii kubwa zaidi katika kabila ya Washona.
Wakaranga ni wa kundi kubwa la Washona na wengi wanahisi ni zamu yao kuingia madarakani kufuatia miaka 37 ya kutawaliwa na kundi la Zezuru atokaye Mugabe.
Wanajeshi wa Zimbabwea waliingilia kati mzozo DR Congo kuisaidia serikali
Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa mataifa wa mwaka 2001, Bw Mnangagwa alionekana kama 'mhandisi wa shughuli za kuingiza fedha za Zanu-PF.'
Hii kwa kiasi kikubwa inahusisha operesheni za jeshi la Zimbabwe na wafanyabiashara katika Jamuhuri Ya Kidemokrasia ya Congo.
Majeshi ya Zimbabwe yaliingilia mzozo wa Congo kwa upande wa serikali, kama ilivyo nchi nyingine, wametuhumiwa kuutumia mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo kuiba utajiri wa maliasili wa nchi hiyo kama vile Almasi, dhahabu a madini mengine.
Lakini licha ya mchango wa kukipatia chama fedha, Bwana Mnangagwa, ambaye ni mwanasheria aliyekulia Zambia, sio mtu anayependwa sana na watu wenye vyeo na wasio na vyeo katika chama chake.
Mmoja wa Maveterani wa vita nchini Zimbabwe, ambaye alifanya naye kazi kwa muda mrefu, anaweka wazi kwa kumuelezea kuwa ni mtu katili.
Mnangagwa alijipatia sifa zake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka ya 1980 kati ya chama cha Zanu chake Robert Mugabe (kushoto) na Zapu chaJoshua Nkomo (kulia)
Afisa mwingine wa ZANU PF aliuliza swali lenye mvuto, wakati alipotaka kujua kuhusu mtazamo wa Bwana Mnangagwa '' Unadhani kuwa Mugabe ni mbaya. Lakini ulifikiri kuwa yoyote atakayekuja badala yake anaweza kuwa mbaya zaidi?''
Mgombea wa upinzani ambaye ambaye alimshinda Bwana Mnangagwa katika kampeni za ubunge mwaka 2000, katika eneo la Kwekwe, Blessing Chebundo anaweza pia kukubaliana kwamba mpinzani wake siye mtu wa amani.
Wakati wa Kampeni kali, Bwana Chebundo alinusurika kifo baada ya vijana wa chama cha ZANU-PF, ambao walimteka na kummwagia petroli, lakini hata hivyo hawakufanikiwa kumchoma.
Ukatili
Sifa za kutisha za Bwana Mnangagwa zilianza wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka miaka ya 80 kati ya chama cha Rais Mugabe cha Zanu na kile cha Joshua Nkomo cha Zapu.
Kama Waziri wa Usalama wa Taifa wa Zimbabwe, Bwana Mnangagwa alikuwa akihusika na Idara ya Usalama wa Taifa, ambayo ilikuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na jeshi kukikandamiza chama cha Zapu.
Maelfu ya raia wasio na hatia, wengi wakiwa kabila la Ndebele, ambao ndio walioonekana kama wafuasi wa Zapu, waliuawa kabla ya vyama hivyo viwili kuungana na kuunda Zanu-PF.
Mnangagwa hapendwi sana na watu wanaofuata sera za Zanu-PF
Miongoni mwa mambo ya ukatili yaliyofanyika ni pamoja na wanavijiji kulazimishwa kucheza huku wakiwa wamenyooshewa bunduki, wakati wa mazishi ya jamaa zao na maneno ya kumuunga mkono Mugabe.
Licha ya makubaliano ya umoja yaliyofikiwa mwaka 1987, bado majeraha ya maumivu yangali yapo. Na watu wa Kabila la Matebele pengine wanaweza kukaidi kumuunga mkono Mnangagwa katika kinyang'anyiro cha Urais.
Amepata Mafunzo China
Bw Mnangagwa ana wafuasi wengi ya waliokuwa katika wakiongoza kampeni ya vita dhidi ya wakulima weupe na wapinzani kutoka mwaka 2000.
Zimbabwe ilipigana vita vya msituni kabla ya kujipatia uhuru 1980
Grace Mugabe (kulia) anaonekana kukumbana na kisiki akikabiliana na Bw Mnangagwa
Wanamkukmbuka kama mmoja wapo wa wanaume,ambaye baada ya mafunzo ya kijeshi China na Misri,alioongoza vita vya kupigania uhuru vya 197.
Maelezo rasmi ya Bw Mnangagwa ni kwamba alikuwa mhanga wa ukatili uliotekelezwa na serikali iliyoongozwa na Wazungu katika taifa la zamani la Rhodesia mwaka 1965.Hii ni baada ya yeye na 'kundi la mamba' alilokuwa analiongoza walisaidia kulilipua treni iliokuwa karibu na eneo la Fort Victoria(ambayo sasa ni Masvingo).0.
Maoni